loader
Picha

NMB yazindua mikopo maalum kwa hospitali, maduka ya dawa

BENKI ya NMB imezindua 'NMB Afya loan', huduma mpya itakayotoa mikopo ya gharama nafuu kwa hospitali binafsi, vituo vya afya, zahanati, wasambazaji na maduka ya dawa nchini.

Ikishirikiana na Shirika la Stichting Medical Credit Fund (MCF), NMB itatoa mikopo kuanzia Sh. milioni bili hadi Sh bilioni tano huku MCF ikitoa dhamana ya asilimia 50 kwa mikopo yote itakayotolewa kupitia huduma hiyo ya kipekee nchini.

NMB Afya Loan inaifanya benki hiyo kuwa taasisi ya kifedha ya kwanza hapa nchini kutoa huduma hiyo ambayo kwa kushirikiana na MCF, ufadhili wa huduma ya afya, kupanua na kuimarisha ubora wa utoaji wa huduma hiyo muhimu kwa wananchi ni sehemu ya matarajio makuu.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Ofisa Mkuu katika kitengo cha Wateja Binafsi, biashara ndogo na za kati, Filbert Mponzi alisema leo Jumanne jijini Dar es Salaam, huduma hiyo ya mikopo imefika kwa wakati mwafaka na utachangia kuongeza upatikanaji wa huduma nafuu za afya na kujenga mifumo endelevu kwasababu upatikanaji wa mitaji unakuwa rahisi zaidi.

“Huduma hii itawawezesha watoa huduma ya afya kupata fedha pamoja na kupata utaalum wa kiufundi, ambao utasaidia kutambua wauzauji na vifaa vya matibabu bora pamoja na upatikanaji wa vifaa vya tiba kwa ajili ya uboreshaji wa huduma zao. Kuna fursa nyingi katika sekta ya afya nchini na sisi kama NMB, tumeliona hili na tumejikita kuwapa nafasi hospitali, vituo vya afya wasambazaji wa vifaa vya tiba kujiendeleza,” Mponzi alinukuliwa.

Naye Mkurugenzi wa MCF Tanzania, Dk Heri Marwa alisema kuanza utekelezaji wa huduma hiyo mpya ni muhimu katika kutimiza malengo ya MCF ya kuhakikisha Watanzania wengi wanapata huduma nafuu za afya na tiba.

"Upatikanaji wa mitaji kwa ajili ya uwekezaji ni changamoto kubwa katika nchi nyingi barani Afrika na inazuia utoaji huduma nafuu za afya hususan tukiangalia mifumo endelevu ya afya. Kwa huduma hii tunafurahi kwamba hospitali nyingi binafsi, vituo vya afya vitapata na uwezo wa kuwekeza kwenye vifaa vya afya vya kisasa,” alisema Dk. Heri Marwa.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi