loader
Picha

‘Tuko tayari kusambaza mifumo ya teknolojia SADC’

JESHI la Polisi Tanzania, Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), limewasilisha mifumo miwili ya teknolojia katika mkutano wa Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na limesema lipo tayari kuipeleka katika nchi zote za jumuiya hiyo zisizo na teknolojia hiyo.

Mifumo hiyo iliyobuniwa na wataalamu wa Tehama wa jeshi hilo nchini, ni wa Usimamizi wa Makosa ya Usalama Barabarani na kupata Taarifa ya Upotevu ya Polisi kwa njia ya mtandao bila kulazimika kwenda kituo cha Polisi.

Jeshi hilo, Kitengo cha Tehama, Makao Makuu, limeifikisha mifumo hiyo katika mkutano huo unaoendelea jijini Dar es Salaam, unaowahusu mawaziri wa sekta ya Tehama, Habari, Mawasiliano, Uchukuzi (Usafirishaji) na Hali ya Hewa kutoa elimu na kueleza utayari wao kuzisaidia nchi nyingine za SADC.

Akizungumza na gazeti hili juzi katika eneo la mkutano huo; Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) walikoweka Banda lao la Jeshi la Polisi, Msimamizi wa Kitengo cha Tehama, makao makuu ya Polisi, Dar es Salaam, Gabriel Mukungu, alisema jeshi hilo lipo tayari kuifikisha mifumo hiyo katika nchi za jumuiya hiyo.

“Tuko hapa kuoneshauwezo wa kiteknolojia wa Jeshi la Polisi. Mifumo hii miwili tuliyoileta hapa imebuniwa na vijana wa jeshi wenyewe, hatujanunua kutoka nje. Hatua hii imesaidia pia kupunguza gharama kwa Jeshi la Polisi na kwa wananchi,” alisema Mukungu.

Akifafanua kuhusu mifu- mo hiyo, akianza na Mfumo wa Usimamizi wa Makosa ya Usalama Barabarani, Mukungu alisema miaka ya zamani wakosaji wa sheria za usalama barabarani wali- andikiwa faini kwa karatasi (vitabu vya notification) vilivyokuwa vinatengenezwa kwa gharama na kulazimika kusafirishwa mikoa yote kwa magari.

Alisema baada ya kuanza kwa mfumo huo Aprili 2017 katika Mkoa wa Pwani na Julai kusambazwa nchi nzima, mabilioni ya Serikali yaliokuwa yakipokea sasa hakuna tena wizi huo kwa kuwa fedha zinapelekwa moja kwa moja serikalini na adhabu imeainisha kosa la dereva na mwenye gari tofuati na awali.

“Sasa hivi mtu akikosa, ana nafasi ya kulipa faini ya kosa lake katika kipindi cha siku saba na kwa wanaokiuka utaratibu huo wanageuka kuwa wadaiwa sugu na hukamatwa kwa kamera maalum zinazowekwa barabarani na kuwabana kulipa faini hizo mara mbili ya faini ya awali (penalty),” alisema Mukungu.

Kuhusu Taarifa ya Upotevu ya Polisi (Police Loss Report), Mukungu alisema umeanza Julai Mosi mwaka huu na unafanya kazi nchi nzima. Alisema mtu aliyepoteza kitu anaingia moja kwa moja kwenye mtandao wa intaneti kwa tovuti ya https://lormis.tpf. go.tz kusajili taarifa zake za upotevu.

“Masharti hapa ni lazima mtu awe na kitambulisho cha taifa. Tumefanya hivi ili kuhimiza kila mwananchi apate kitambulisho hiki kuonesha umuhimu wake. Kwa hiyo kama umepo- telewa na nyaraka kama vyeti, laini ya simu na kadi za benki, hana ulazima wa kwenda Kituo cha Polisi, anaweza kuipata ‘loss re- port’ mtandaoni,” alisema.

Akieleza zaidi, Mukungu alisema gharama ya kuipata ni Sh 500 kiasi ambacho watu wengi wanaweza kukipata kwa njia ya simu ya mkononi. Hata hivyo, alisema mtu hatopata taarifa ya upotevu kwa vitu kama kadi ya gari, gari lenyewe na vyombo vya moto, hati za nyumba, mashamba, kampuni, silaha, kifo na mtu kupotea kwa kuepuka hatari ya mwizi wa vitu husika, hawajaziweka mtandaoni kuepuka matumizi mabaya na watu kujihalalishia vitu hivyo.

“Kwa aina hii ya upotevu, mtu atalazimika kwenda kituo cha polisi”. Alisema hivi sasa wanaunganisha mifumo hiyo na kampuni za simu ili kurahisisha taarifa kuwafikia kampuni hizo mara moja kama zinavyowafikia Polisi.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi