loader
Picha

Majaliwa: Siridhishwi na gawio Kilombero Sugar

WAZIRI Mkuu Kassimu Majaliwa amesema haridhishwi na gawio la Sh milioni 800, linatolewa na viwanda vya sukari vya Kilombero, ikilinganishwa na gawio la Sh bilioni 15 zinazotolewa na Kiwanda cha Sukari cha Moshi (TPC ).

Kutokana na hatua hiyo, Waziri Mkuu amevitaka viwanda hivyo kuhakikisha kuwa vinaongeza kiwango cha gawio kwa serikali. Majaliwa alisema hayo jana wakati alipotembelea Kiwanda cha Sukari cha Kilombero na kukutana na uongozi na wafanyakazi wa kiwanda hicho.

Pia alivitaka viwanda vya sukari nchini kuhakikisha vinazalisha sukari nyingi ili kukidhi mahitaji ya ndani na kuepuka kuagiza sukari nje ya nchi ambayo nyingine haina ubora. “Ni lazima tuhakikishe tunazalisha sukari ya kutoka, hii itasaidia kuondokana na uingizwaji wa sukari kutoka nje,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.

Alisema serikali iliamua kutoa ruhusa ya viwanda kuagiza sukari nje ili kudhibiti ujanja, uliokuwa unafanywa na baadhi ya wafanyabiashara, waliokuwa wakiagiza sukari kutoka nje ya nchi kiholela na nyingine kukosa ubora.

Alisema bado kuna uhi- taji mkubwa wa sukari za viwandani, hatua inayoilazimu serikali kutoa vibali kwa wamiliki wa viwanda kuagiza nje. Alivitaka viwanda hivyo vya ndani vya sukari ku- jikita pia katika kuzalisha sukari ya viwandani ili kukabiliana na upungufu huo.

Alipongeza uongozi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero, kwa mpango wake wa kutaka kuanzisha kiwanda cha kuzalisha sukari ya viwandani. Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba alisema mahitaji ya sukari mwaka huu, yaliongezeka hadi kufikia tani 710,000 ikilinganishwa na mwaka jana, ambapo mahitaji yalikuwa tani 610,000.

Alisema ongezeko hilo limetokana na kuongezeka kwa viwanda vipya, vinavyotumia sukari ya viwandani ambapo mahitaji yake ni tani 165,000. Alisema mahitaji halisi ya sukari ya nyumbani kwa sasa ni tani 545,000, ambapo kiwanda cha Kilombero kinazalisha tani 134,000, Kiwanda cha Manyara tani 6,000, Kiwanda cha Mtibwa tani 39,000 na TPC cha Moshi tani 100,000.

WANAWAKE wenye matatizo ya Fistula nchini wametakiwa kuacha kujifungia ndani ...

foto
Mwandishi: John Nditi, Kilombero

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi