loader
Picha

NACTE yafungua tena dirisha la udahili

BARAZA la Taifa la Elimu ya Juu (NACTE) limewataka wahitimu wa kidato cha nne na sita, walio na sifa za kujiunga na programu mbalimbali, kutumia muda wa wiki moja iliyobaki, kutuma maombi ya udahili kwenye vyuo na taasisi mbalimbali za ualimu zinazosimamiwa na baraza hilo, kabla ya kufungwa kwa dirisha hilo.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Kitengo cha Udahili wa NACTE, Twaha Twaha, alisema hatua hiyo imetokana na uwepo wa nafasi katika baadhi ya vyuo, ambapo majina ya wadahiliwa 58,193 waliochaguliwa kwa ajili ya kujiunga na vyuo mbalimbali yanaendelea kuhakikiwa.

Alisema kutokana na hatua hiyo ya baadhi ya wahitimu, kukosa nafasi katika vyuo vya afya na elimu vya serikali vinavyotajwa kuwa vimejaa, bado kuna nafasi katika baadhi ya vyuo na taasisi nyingine za binafsi zenye nafasi.

Kwamba kwa kuzingatia hilo, wameona vyema kutangaza nafasi ya pili ya udahili ili kuwawezesha wahitimu waliokosa kuom- ba nafasi ya kudahiliwa. “NACTE ilifungua dirisha la udahili kwa awamu ya pili na ya mwisho kwenye vyuo na taasisi zinazotoa programu za Astashahada na Stashahada hapa nchini kuanzia Septemba 7, mwaka huu na kutarajiwa kulifunga ifikapo Septemba 25, hivyo ni vyema waombaji wakatumia muda wa siku hizi zilizobaki kukamilisha maombi hayo,” alisema Twaha.

Alisema majibu ya uhakiki ya wale watakaochaguliwa na taasisi na vyuo mbalimbali nchini, yatawasilishwa NACTE kuanzia Septemba 25 hadi 27 mwaka huu, huku majibu ya uhakiki kutoka NACTE kwa wale waliopata nafasi, yanatarajiwa kutolewa Oktoba 4, mwaka huu.

Twaha aliwataka wahitimu hao kuhakikisha wanaitumia nafasi hiyo pekee, kwa kuwa hakutakuwa na nafasi nyingine baada ya hiyo. Aliwataka waombaji kutopoteza muda wao kuomba nafasi katika vyuo, ambavyo tayari nafasi zimejaa.

JESHI la Polisi mkoani Manyara linawashikilia watu wanne wanaotuhumiwa kumteka ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

1 Comments

  • avatar
    enock john
    18/09/2019

    mbona link ya kuingilia haipo toka wafungue dirisha lao tarehe7 mpk sasa ivi hatuoni chochote

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi