loader
Picha

Kishindo cha JPM chaleta kizaazaa Vingunguti, Coco Beach

‘MCHELEA mwana kulia, hulia mwenyewe.’ Ndivyo unavyoweza kusema baada ya viongozi wa Jiji la Dar es Salaam na Shirika la Nyumba la Taifa (NHC), kuamua kuchukua hatua za haraka za kuanza ujenzi wa machinjio ya Vingunguti.

Hatua hiyo imekuja baada ya Rais John Magufuli, kutembelea machinjio hiyo juzi na kutoa maagizo ya kuwataka viongozi hao kuanza ujenzi wa machinjio hiyo haraka. Aidha kishindo cha ziara ya Rais Mgufuli katika Machinjio ya Vingunguti juzi, pia kimetikisa Ufukwe wa Coco, baada ya Manispaa ya Kinondoni kutangaza kuufunga ufukwe huo kwa muda wa miezi 6 kuanzia jana ili kupisha uboreshaji wa ufukwe huo.

Jana gazeti hili lilishuhu- dia harakati zinazoonesha kuwa viongozi hao, wameamka na kuamua kupiga kambi katika eneo hilo ili kuhakikisha wanatekeleza haraka ujenzi huo, huku wakiahidi kukamilisha ndani ya muda ulioagizwa na Rais Magufuli.

Katika ziara yake ya kushitukiza katika eneo hilo juzi, Rais Magufuli alionekana kukerwa na hali mbaya ya machinjio hayo, ambayo licha ya kutengewa Sh bilioni 12.5 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la kisasa hakuna kilichofanyika hadi sasa.

Jana gazeti hili lilitembelea katika eneo hilo na kuwakuta viongozi mbalimbali akiwemo Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Abubakari Kunenge, Mkurugenzi Mkuu wa NHC Dk Maulid Banyani, Meya wa Manispaa ya Ilala, Omary Kumbilamoto na viongozi wengine kutoka ofisi mbalimbali za serikali wakiwa katika eneo hilo na kujadiliana hatua muhimu kuhusu ujenzi huo.

“Nafikiri mliona namna Rais alivyotuagiza jana (juzi), hatuna muda wa kusubiri kikubwa hapa tunakutana na kuweka mipango ya kuanza haraka ujenzi huo ili kutekeleza agizo lake la ku- kamilisha machinjio hii katika muda aliousema.

“Kuanzia sasa nitakuwa hapa kila siku hata ikibidi kulala hapa hadi ujenzi utakapomalizika,” alisema Kunenge. Alisema hawaoni sababu ya kuendelea kuchelewa kutekeleza ujenzi huo, kwa kuwa agizo la Rais Magufuli lina uzito mkubwa kwao.

Kwamba wanatarajia kuona ujenzi wa machinjio hiyo unakamilika ifikapo Desemba kama walivyoagizwa. Alisisitiza kuwa watafanya kazi usiku na mchana hadi ujenzi huo utakapokamilika. Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa NHC, Dk Banyani alisema anaamini wataweza kulitekeleza agizo hilo la Rais la kukamilisha ujenzi huo ifikapo Desemba ,kwa kuwa wana nyenzo zote kufanikisha ujenzi ikizingatiwa kuwa fedha za ujenzi tayari zimeshatolewa Alisema kuanzia sasa wameamua kupiga kambi katika eneo hilo, ikibidi hata kulala katika eneo hilo ili kufanikisha ujenzi huo uliopo katika Kitalu No 3003 na 3004 Block ‘ B’eneo la Vingun- guti ndani ya Manispaa hiyo ya Ilala unaotekelezwa na shirika lake.

Rais Magufuli aliwaagiza viongozi hao, kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo ifikapo Desemba mwaka huu. Aliahidi kurudi tena katika eneo hilo ndani ya kipindi hicho kwa ajili ya kujiridhisha na ujenzi huo. Aliwataka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda na viongozi wa Jiji kuacha maneno na badala yake wafanye kazi kwa vitendo.

Aliwataka viongozi hao kuwa na timu ya kutosha, ikiwezekana hata kuwaita wanajeshi ili kukamilisha ujenzi huo haraka, badala ya miezi 18 kama ambavyo wamekubaliana na mkanda- rasi anayejenga machinjio hiyo.

Pia aliwataka viongozi hao kuacha kukusanya ushuru katika eneo hilo hadi pale ujenzi wa machinjio hayo, utakapokamilika. Alihoji inakuwaje wanakusanya fedha katika eneo ambalo ni chafu kimazingira.

Aliwataka wafanyabiashara kutolipa hata senti. Gazeti hili liliwashuhudia mafundi wakiendelea na shughuli mbalimbali za maandalizi ya ujenzi huo, ikiwemo uunganishaji wa taa katika uzio unaozunguka eneo hilo tayari kuwezesha ujenzi huo kuanza.

Ufukwe wa Coco Kishindo cha ziara ya Rais Mgufuli katika Machinjio ya Vingunguti juzi, pia kimetikisa Ufukwe wa Coco, baada ya Manispaa ya Kinondoni jana kutangaza kuufunga ufukwe huo kwa muda wa miezi sita kuanzia jana ili kupisha uboreshaji wa ufukwe huo.

Kutokana na hatua hiyo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Aron Kagurum- juli, amewataka wafanyabi- ashara wa eneo hilo, watafute ufukwe mwingine kwa sasa.

JESHI la Polisi mkoani Manyara linawashikilia watu wanne wanaotuhumiwa kumteka ...

foto
Mwandishi: Oscar Job

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi