loader
Picha

Watumishi wala rushwa kuendelea kutumbuliwa

SERIKALI imeahidi kuendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa watumishi, watakaojihusisha na Avitendo viovu vya rushwa. hadi hiyo imetolewa Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga wakati akifungua kikao kazi jijini Dodoma jana.

Kikao hicho kiliwakutananisha wenyeviti wa bodi na taasisi za wizara hiyo, wakurugenzi na watendaji wakuu wa bodi na taasisi. Kilijadili utekelezaji wa mikakati waliyojiwekea.

Hasunga alisema kuwa serikali inayoongozwa na Rais John Magufuli, imejipambanua kukabiliana na wala rushwa. Hivyo, yeyote anayebainika, hakutakuwa na huruma, badala yake atapelekwa mahakamani.

“Wenyeviti na wakuru- genzi msipoisaidia serikali kuchukua hatua dhidi ya watumishi wanaotoa au kupokea rushwa, maana yake na ninyi ni sehemu ya wala rushwa ;na kama sio sehemu lazima tuchukue hatua,” alisema.

“Nimeyasema haya hadharani, sina lengo la kumtishia mtu yeyote katika hili, badala yake nimelisema ili hatua zichu- kuliwe,” alisema. Hasunga alisema kuwa wizara yake itapimwa katika mambo makubwa matano, ambayo ni kuongeza uzalishaji wa chakula na tija katika kilimo ili kuimarisha usalama wa chakula na lishe.

Jambo la pili ni kwa namna gani wizara imewezesha upatikanaji wa fedha za kigeni. Jambo la tatu ni kupimwa kuwa kilimo kinakua kwa asilimia ngapi na kinachangia kiasi gani kwenye pato la Taifa.

Mambo mengine ni upatikanaji wa malighafi sahihi kwa ajili ya viwanda nchini, idadi ya ajira zitakazopatikana kwenye kilimo na namna ushirika utakavyoimarika na usimamizi madhubuti wa ardhi kwa ajili ya kilimo, hususani kilimo cha umwagiliaji.

Alisema kuwa endapo maeneo hayo matano yatafanyiwa kazi ipasavyo ni wazi kuwa serikali kupitia wizara ya kilimo itakuwa imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kabisa kukibadilisha kilimo kuwa cha kibiashara na sio cha kujikimu.

Hasunga alisema kuwa maendeleo ya Sekta ya Kilimo na Tasnia ya Ushirika nchini, yataimarika baada ya kuzinduliwa mfumo rasmi wa mauzo ya mazao ya kilimo kupitia Soko la Bidhaa Tanzania (TMX).

TMX ina lengo la kuongeza ufanisi katika juhudi za serikali za kurasimisha mifumo ya masoko, ambayo imekuwa na changamoto kwa muda mrefu kwa kuwaunganisha wauzaji na wanunuzi wa bidhaa, kuleta ushindani kwenye bei, kupunguza gharama za uendeshaji biashara na kuweka uwazi.

JESHI la Polisi mkoani Manyara linawashikilia watu wanne wanaotuhumiwa kumteka ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi