loader
Picha

Vijana wafufua suala la mgombea binafsi

BAADHI ya vijana wamesema mfumo wa sasa wa kuteuliwa kugombea kupitia vyama vya siasa, umekuwa ukiwabana watu wengi hususani vijana, na kusisitiza haja ya kuwa na mgombea binafsi.

Akizungumza wakati wa mjadala juu ya changamoto, zinazowakabili vijana wakati wa uchaguzi, ulioandaliwa na Shirika la Maendeleo ya Vijana Kibaha (YPC), mmoja wa washiriki, Adolphus Mushumbusi alisema mfumo wa wagombea kuteuliwa na vyama, umekuwa ukiwabana wengi.

“Kwa sasa ndani ya vyama vya siasa, kuna changamoto ya vijana kutopewa fursa ili kugombea katika nafasi mbalimbali zikiwamo za udiwani na ubunge, vyama vimekuwa haviwaamini vijana, nafasi nyingi bado zinachukuliwa na wazee, jambo ambalo linafanya vijana kushindwa kutimiza ndoto zao,” alieleza.

Alisema njia pekee ya kutoa fursa kwa vijana kugombea nafasi mbalimbali ni kuanzishwa mfumo wa mgombea binafsi. Alisema kuwa mfumo wa mgombea binafsi, utawa saidia vijana kupata fursa ya kugombea na kupenya katika nafasi mbalimbali, zitakazowasaidia kutimiza ndoto zao.

Mtoa mada katika mjadala huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa la Katiba (JUKATA), Hebron Mwakagenda aliomba serikali kuangalia namna ya kufanya siku ya kupiga kura kuwa maalumu ili watu wengi washiriki kwenye uchaguzi.

“Nchi kama Kenya na Zambia marais wao hutangaza siku ya kupiga kura na siku hiyo hakuna shughuli nyingine zaidi ya kupiga kura ili kuwapa watu wengi fursa ya kuchagua viongozi wao,”alisema Mwakagenda.

Alisema mfumo unaotumika hapa nchini wa kupiga kura siku ya Jumapili, ume- kuwa ni moja ya changa- moto kwa watu wengi kush- indwa kupiga kura kutokana na kuwa makanisani.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi