loader
Picha

Amzuia bintiye kufanya mtihani la 7, amuoze

Polisi Wilaya ya Nkasi mkoani Rukwa inamshi kilia mkazi wa kijiji cha Paramawe kilichopo katika Kata ya Mtenga wilayani humo, Luvinza Kasakwa (55) akituhumiwa kumzuia binti yake asifanye mtihani wa kumaliza elimu ya msingi, ili amuoze.

Msichana huyo mwenye umri wa miaka 16 alikuwa akisoma katika Shule ya Msingi Paramawe iliyopo katika Kata ya Mtenga iliyopo katika wilaya ya Nkasi. Taarifa kutoka ndani ya Jeshi la Polisi Wilaya ya Nkasi zinaeleza kuwa mtuhumiwa atafikishwa mahakamani wakati wowote baada ya upelelezi wa shauri lake kukamilika.

“Sakata la kukamatwa mtuhumiwa Kasakwa ni la kweli lakini siwezi kueleza kwa undani kwa sababu mimi si msemaji “alieleza mmoja wa maofisa wa Polisi kutoka Kituo cha Polisi wilaya ya Nkasi kilichopo katika mji mdogo wa Namanyere.

Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu yaliyofanyika kwa njia ya simu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi, Missana Kwangura amekiri kutokea tukio hilo.

Akisimulia kwa undani, alisema Septemba 12, mwaka huu ambayo ilikuwa siku ya kwanza ya wanafunzi wa darasa la saba kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi, mwanafunzi huyo hakuonekana katika chumba cha mtihani katika Shule ya Msingi Paramawe.

“Mtihani wa kwanza uli- kuwa wa somo la Kiinger- eza lakini msichana huyu hakuwepo kwenye chumba cha mtihani, Msimamzi wa mtihani alitoa taarifa kwa Ofisa Mtendaji wa Kata ambaye aliwasiliana na mzazi wa kiume wa mwanafunzi huyo ambaye alidai kuwa binti yake alikuwa mgonjwa,”alisema.

Baada ya kushawishiwa kwa simu alikubali kumpeleka binti yake shuleni hapo, lakini alipofika alionekana dhahiri kuwa hakuwa mgonjwa, hivyo aliamriwa kuingia kwenye chumba cha mtihani lakini alikuwa amechelewa hakufanya mtihani wa somo la Kiingereza, mengine yote manne alifanya.

Baba mzazi wa msichana huyo alikamatwa na kushikiliwa katika Kituo cha Polisi kilichopo katika Kata ya Paramawe kabla ya kuhamishiwa wilayani. “Japo hatuna ushahidi wa moja kwa moja lakini kuna uwezekano mkubwa kuwa baba mzazi wa msichana huyo alikuwa na nia mbaya ya kusababisha binti yake asifanye mitihani ili amuoze,” alisisitiza Diwani wa Kata ya Mtenga, Pancras Malyatabu akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu alisema kuwa msichana huyo alipohojiwa alikiri kuwa hakuwa mgonjwa, huku akisisitiza kuwa baba yake mzazi alimtaka afanye vibaya mtihani wake ili amuozeshe na baadaye alimzuia kabisa asifanye mtihani huo.

WANAWAKE wenye matatizo ya Fistula nchini wametakiwa kuacha kujifungia ndani ...

foto
Mwandishi: Peti Siyame, Sumbawanga

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi