loader
Picha

Kesi ya Kisena yaendelea kupigwa kalenda

Kesi ya uhujumu uchumi inyomkabili Mkurugenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (UDART), Robert Kisena (46) na wenzake wanne katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,imeendelea kupigwa kalenda kwa sababu upelelezi bado haujakamilika.

Wakili wa Serikali, Saada Mohammed alidai mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile kuwa washitakiwa wote wapo na kesi hiyo imekuja kwa ajili ya kutajwa. Alidai upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika, hivyo aliomba tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.

Hakimu Rwizile aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 30, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa na washitakiwa wamerudishwa rumande kwa sababu mashitaka hayo hayana dhamana kisheria.

Mbali na Kisena washitakiwa wengine ni mkewe Florencia Membe, Kulwa Kisena(33), Charles Newe(47) na raia wa China, Cheni Shi (32) ambao kwa pamoja wanawakilishwa na Wakili Nehemia Nkoko. Washitakiwa wanakabiliwa na mashitaka 19 ikiwemo kusababisha hasara kwa UDART ya Sh bilioni 2.41.

Katika mashitaka hayo yapo ya kuongoza genge la uhalifu, kujenga kituo cha mafuta bila kibali, kuuza mafuta sehemu zisizoruhusiwa, wizi wa mafuta na utakatishaji fedha wa Sh bilioni 1.2, kughushi na kusababisha hasara ya Sh bilioni 1.4.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi