loader
Picha

Katiba TAFF kupatikana ndani ya siku 30

Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) linatekeleza mchakato wa marekebisho ya katiba na limetoa siku 30 kwa wadau na wanatasnia ya filamu nchini kutoa maoni yao kwa rasimu ili kuwa na katiba yenye tija kwa tasnia hiyo.

Rasimu ya TAFF iliundwa na kupelekwa kwa wadau na baada ya kikao cha utendaji kazi kati ya Bodi ya Filamu Tanzania, Basata na TAFF, ikaazimiwa upatikanaji wa katiba. Rais wa TAFF, Simon Mwakifamba, alisema hayo jana Dar es Salaam na kuongeza kuwa, ukusanyaji maoni utajumuisha wadau mbalimbali na wanatasnia ili kuboresha sekta ya filamu nchini.

“Nitoe mwezi mmoja tu tangu siku ya leo (jana). Rasimu itapatikana kupitia njia mbalimbali iki- wamo kwenye ukurasa maalum wa Facebook, kusambazwa kwa njia mbalimbali za mitandao,” alisema Mwakifamba.

Alisema baada ya kupokea maoni, kupitia kikao cha bodi, TAFF itaitisha mkutano mkuu wa wanachama wake kwa ajili ya ajenda kuu moja kisha kuipitisha ama kuikataa rasimu ya katiba hiyo pendekezwa.

Alisema TAFF inawaomba wote wenye nia njema wasisite kutoa mawazo yao ili kuujenga umoja huo wa wenye tasnia ya filamu Tanzania ili kuifanya kuwa yenye mchango katika sa- fari ya Tanzania kuwa na uchumi wa kati kufikia mwaka 2025.

Mbali na wadau kutakiwa kutoa maoni ya rasimu ya katiba, alisema TAFF inajivunia kuipi- gania Sera ya Filamu Tanzania tangu mwaka 2014 kwa kiasi na serikali imeshatoa ahadi kwamba kabla mwaka huu haujaisha ita- kuwa tayari imeshapatikana.

Alisema pia katika sekta ya sanaa bunifu, shirikisho hilo linaendelea kufanya utafiti kuhusu sera ya miliki bunifu (IP) ambayo inalenga kuwa na maboresho makubwa katika tasnia ya filamu.

Alisema shirikisho hilo lilianzishwa na wadau wa tasnia ya filamu Tanzania, kisha kupewa baraka za utendaji kazi kwa usajili namba BST 4536 wa mwaka 2010 wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) linalofanya kazi chini ya sheria ya serikali ya uendeshaji wa Tasnia ya sanaa nchini namba 4 ya mwaka 1984.

BOSTON Marathon sasa imefutwa kabisa ikiwa ni mara ya kwanza ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi