loader
Picha

Mwakyembe amlilia mwandishi Dilunga

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk Harrison Mwakyembe ametuma salamu za rambirambi kwa familia ya aliyekuwa Mhariri wa Habari wa gazeti la Jamhuri Godfrey Dilunga aliyefariki dunia jana, Jumanne alfajiri.

Dk Mwakyembe ameeleza kuwa kifo cha Dilunga ni pigo kubwa kwa tasnia ya habari na michezo ikizingatiwa kuwa amewahi kuwa mwanakamati wa Masoko na Habari katika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

“Kwa hakika tumepoteza mtu muhimu sana katika tasnia yetu ya habari na michezo, Mungu awape nguvu wanafamilia wote,” ameeleza.

Enzi za uhai wake Dilunga amewahi kufanya kazi na gazeti la Raia Mwema na Mtanzania akiwa mmoja wa wahariri wa magazeti hayo.

Dk Mwakyembe ametoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki na tasnia ya habari kufuatia msiba huo.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Na JANETH MESOMAPYA

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi