loader
Picha

Aliyeua kwa kudanganywa na sangoma ahukumiwa kifo

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Mbeya imewahukumu kunyongwa hadi kufa watu wanne kutoka wilayani Mbozi mkoani Songwe, baada ya watatu kati yao kukutwa na hatia ya kuua kwa kukusudia ili kuiba Sh milioni moja ;na mmoja kuua na kuchukua viungo vya sehemu za siri za marehemu na kupeleka kwa mganga wa kienyeji.

Katika hukumu ya kwanza, mahakama hiyo imemhukumu kunyongwa hadi kufa, Aman Kalinga (23), mkazi wa Kijiji cha Mpanda Kata ya Nyimbili kwa kumuua Heroni Kalinga (13) na kuchukua viungo vyake vya siri na kupeleka kwa mganga wa kienyeji, aliyefahamika kwa jina moja la Makamu.

Katika hukumu ya pili, Nathan Elias, Moses Kasitu na Elias Mzumbwe wakazi wa wilayani Mbozi, walitiwa hatiani na mahakama hiyo kwa kushiriki kumuua Vasko Njowela, aliyekuwa akifanya kazi ya kuuza duka katika eneo la Mpemba Tunduma wilayani Momba na kupora Sh milioni moja. Tukio hilo lilitokea saa 1:30 usiku Julai 25 mwaka 2014 wakati muuza duka huyo akiwa getini kuingia nyumbani kwa mwajiri wake.

Hakimu wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya, Dk Adam Mambi alisema kitendo hicho ni kinyume cha kifungu cha sheria. Akitoa hukumu, alisema mahakama imejiridhisha pasipo kuacha shaka yoyote kufuatia ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, kuwa watu hao walitenda kosa hilo la mauaji.

Alisema imethibitika kuwa watuhumiwa walimvamia Njowela wakati akiingia getini nyumbani kwa bosi wake akitoka dukani, wakiwa na lengo la kumpora begi ambalo aliweka fedha hizo.

Alisema mara baada ya kumvamia muuza duka huyo, ulizuka ugomvi baina yake na mshitakiwa namba moja Nathan. Mshitakiwa namba mbili, Kasitu aliungana na mshitakiwa namba moja kumshambulia Njowela kisha mshitakiwa namba tatu, Mzumbwe alimpiga muuza duka huyo tumboni kwa bunduki.

Alisema mshitakiwa namba moja, Nathan aliendelea kumkata mapanga Njowela, jambo lililosababisha apoteze uhai. Jaji Mambi alisema upande wa mashitaka ulikuwa na mashahidi 10, akiwemo Rehema Saidi aliyekuwepo kwenye eneo la tukio wakati washitakiwa wakifanya mauaji hayo, ambapo aliamuriwa alale chini baada ya washitakiwa kupiga risasi juu huku wakiendelea na mauaji hayo na uporaji wa fedha.

Alisema baada ya polisi kuwakamata wahusika wa tukio hilo, shahidi huyo aliwatambua wawili kati yao, ambao ni mshitakiwa namba mbili Kasitu, mkazi wa Kilimahewa na mshitakiawa namba tatu Mzumbwe, mkazi wa Ihanda. Aliwatambua baada ya kupitishwa kwenye gwaride la utambuzi lililowashirikisha watu 12.

Alisema ushahidi wa kimaabara, pia ulithibitisha kuwa maganda ya risasi yaliyookotwa eneo la tukio, ndio yaliyotumika katika silaha aliyokamatwa nayo Nathan akiwa Njombe, baada ya washitakiwa wenzake kueleza mahali alipo.

Aliongeza pia kuwa maelezo ya awali waliyoyatoa polisi, yanaonesha kuwa washitakiwa hao walikiri kuhusika na tukio hilo na katika matukio mbalimbali katika mkoa wa Songwe.

Watu hao walikuwa wakitumia short gun yenye namba 007700112. Waliieleza mahakama kuwa hununua risasi nchini Zambia.

MSIMU wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2019/2020 utarejea tena Juni ...

foto
Mwandishi: Na Baraka Messa

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi