loader
Picha

Kabendera aieleza mahakama tatizo lake la kiafya

MWANDISHI wa Habari za Uchunguzi, Erick Kabendera ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam kuwa Hospitali ya Rufaa ya Amana, Dar es Salaam imebaini ana matatizo ya pingili za mgongo, baada ya kumfanyia vipimo mbalimbali ikiwemo vya damu na X-Ray.

Alieleza hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile na kuweka wazi kuwa alipelekwa hospitalini hapo juzi. Kwamba anaendelea na matibabu huku akisubiri vipimo vingine, alivyoelezwa kuwa vitakuwa tayari mwishoni mwa wiki hii. Alidai vipimo vya awali vinaonesha ana tatizo katika pingili za mgongo na ana maumivu makali.

Baada ya kueleza hayo, Wakili wa Utetezi, Jebra Kambore aliuomba upande wa mashitaka kuharakisha upelelezi wa kesi hiyo. Hakimu Rwizile aliahirisha kesi hiyo hadi Oktoba Mosi mwaka huu, kwa ajili ya kutajwa na mshitakiwa amerudishwa rumande.

Kabendera alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Agosti 5, mwaka huu akikabiliwa na mashitaka matatu, ambayo ni kuongoza genge la uhalifu, kukwepa kodi na kutakatisha zaidi ya Sh milioni 173.2.

Katika kesi ya msingi, Kabendera anadaiwa katika siku tofauti kati ya Januari 2015 na Julai, mwaka huu katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam, alitoa msaada katika genge la uhalifu kwa nia ya kujipatia faida.

Inadaiwa siku na mahali hapo mshitakiwa bila kuwa na sababu za msingi kisheria, alishindwa kulipa kodi ya Sh. 173, 247,047.02 ambayo ilitakiwa ilipwe kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Inadaiwa kati ya Januari 2015 na Julai mwaka huu ndani ya Jiji na Mkoa wa Dar es Salaam, mshitakiwa alijipatia kiasi hicho cha Sh milioni 173.2 wakati akijua kuwa fedha hizo ni mazao ya makosa tangulizi ya kukwepa kodi na kujihusisha na genge la uhalifu.

MSIMU wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2019/2020 utarejea tena Juni ...

foto
Mwandishi: Na Francisca Emmanuel

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi