loader
Picha

Serikali yavunja rekodi uunganishaji umeme wananchi

SERIKALI ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Rais John Magufuli imevunja rekodi kwa kuunganishia umeme wananchi 949,000 kwa kipindi cha miaka mitatu, ikilinganishwa na idadi ya wananchi milioni 1.3 waliounganishiwa huduma hiyo miaka 50 iliyopita baada ya Uhuru.

Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu, alipokuwa akizindua uwashaji umeme kwenye kitongoji cha Kisasa, kata ya Tambani, wilaya ya Mkuranga na kueleza kuwa, lengo ni kuhakikisha umeme unamfikia kila mwananchi.

Alisema idadi hiyo imefikiwa kupitia miradi mbalimbali ya umeme ikiwamo inayosimamiwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA), Ujazilizi na Tanesco, lengo likiwa ni kuwafikia wananchi wote wa Tanzania ifikapo 2021.

“Awamu hii ya tano chini ya Rais Magufuli imedhamiria wananchi wote kupata nishati ya umeme kwani umeme ni maendeleo na kwa miradi mingi ambayo inaendelea malengo ya nchi nzima yatafikiwa ifikapo 2021,” alisema Mgalu.

Alisema mradi wa umeme katika miji iliyo pembezoni ambao utawafikia wananchi 4,293 wa awali, Tanesco imetenga kiasi cha Sh bilioni 3.3 kwa mwaka wa fedha 2019/2020.

“Mradi huu utavifikia vijiji 11 na vitongoji 30, ambapo REA Awamu ya Tatu mzunguko wa pili utaanza Desemba, mwaka huu na mradi wa Ujazilizi awamu ya pili utahusisha mikoa tisa,” alisema.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Uvuvi na Mifugo na Mbunge wa Jimbo la Mkuranga, Abdala Ulega, alisema wakati anaingia kwenye nafasi hiyo umeme ulikuwa katika vijiji visivyozidi 10, lakini kwa sasa vimefika vijiji 43.

Alisema licha ya vijiji hivyo kuwa na umeme katika kata za Panzuo, Visegese, Njianne, Kitomondo, Magawa, Bupu na Mchonga, lakini pia mwaka huu huduma hiyo itapelekwa katika vijiji na kata zote.

Kwa upande wake, Meneja wa Tanesco Wilaya ya Mkuranga, Octavian Mmuni, alisema umeme uliowekwa kwenye kata ya Tambani una njia kubwa ya kilometa sita na njia ndogo yenye urefu wa kilometa 11 na utawafikia watu 101 ambao wameshalipia.

Alisema mradi huo una thamani ya zaidi ya Sh milioni 400 na umefikia asilimia 96.

MSIMU wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2019/2020 utarejea tena Juni ...

foto
Mwandishi: Na John Gagarini

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi