loader
Picha

Vifaa vya kisasa vyaokoa maisha ya Askofu

VIFAA vya kisasa vya tiba ya mishipa ya fahamu Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) vimeokoa maisha ya Askofu Mkuu wa Jimbo Katoliki la Dar es Salaam, Mhashamu Thadeus Ruwa’Ichi aliyeanza mazoezi ya viungo.

Profesa Joseph Kahamba, daktari bingwa wa upasuaji wa magonjwa ya ubongo, mgongo na mishipa ya fahamu alisema hayo Dar es Salaam jana. Alisema serikali imefanya uwekezaji mkubwa katika vifaa vya kisasa katika taasisi hiyo kitu ambacho kinaokoa maisha ya watu wengi.

“Upasuaji tuliofanya wa baba askofu ni mkubwa sana, ambapo tulifungua ubongo wake na sasa tunashukuru anaendelea vizuri, anaweza kuongea, anatembea na ameanza mazoezi ya kuchangamsha mwili.

Na hili limewezekana kwa sababu tunavyo vifaa vya kisasa,”alisema. Alisema upasuaji huo umeokoa shilingi bilioni 1.5 ambazo zingetumika kumtibu nje, lakini MOI gharama zake hazizidi Sh. milioni sita. Mwaka 2017 Serikali ilitoa Sh. bilioni 16.5 ili kufunga mashine za kisasa za radiolojia na mashine za CT Scan, MRI, X-Ray mbili, C-Arm na Ultrasound na kuongeza vitanda vya chumba maalum cha uangalizi kutoka vinne hadi 32.

Wiki iliyopita Rais John Magufuli aliahidi kuipa MOI Sh bilioni 1.5 kuongeza vifaa zaidi vya kisasa.

Askofu huyo alihamishiwa Moi Septemba 9 mwaka huu kutoka Moshi, Kilimanjaro na kufanyiwa upasuaji kuondoa damu iliyovilia kwenye ubongo.

Upasuaji huo uliongozwa na Profesa Kahamba na jopo la madaktari bingwa wakiwemo wa usingizi, magonjwa ya ndani, wataalam wa lishe, wauguzi wabobezi na wa mazoezi tiba.

“Tumefarijika jamii inamwombea baba askofu ampone haraka. Kwa maendeleo ambayo anaonyesha anaendelea vizuri. Tuendelee kumwombea, madaktari tunafanya kwa uwezo wetu, mengine tumuachie Mungu, “ alisema.

MSIMU wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2019/2020 utarejea tena Juni ...

foto
Mwandishi: Na Vicky Kimaro

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi