loader
Picha

Godfrey Dilunga kuagwa Mnazi Mmoja leo

WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe ataongoza waandishi, ndugu, jamaa na marafiki kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mhariri wa gazeti la Jamhuri, Godfrey Dilunga (43).

Mwili wa marehemu Dilunga utaagwa leo katika viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam na baadaye utasafirishwa kwenda Morogoro kwa maziko yatakayofanyika kesho.

Mkurugenzi Mtendaji wa Jamhuri Media Limited, Deodatus Balile alisema mwili wa marehemu Dilunga utawasili viwanja vya Mnazi Mmoja saa nne asubuhi taray kwa kuagwa.

Alisema mbali na Waziri Mwakyembe, pia salamu mbalimbali za pole zitatolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk Hassan Abbas, Jukwaa la Wahariri (TEF) na wawakilishi wa vyama vya siasa na wengine.

Wengine ni Baraza la Habari Tanzania (MCT), Shirikisho la Klabu za Waandishi wa Habari (UTPC), Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa), Bodi ya Mikopo Elimu ya Juu (HESLB), Waandishi wa Habari za Bunge, majirani, madhebu ya dini, na baba yake mzazi. Balile alisema safari ya Morogoro kwa maziko ya Dilunga itaanza saa saba kamili mchana.

Dilunga alilazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Septemba 9, mwaka huu kwa rufaa kutoka Hospitali ya Mwananyamala kwa tatizo la maumivu ya tumbo.Alifariki dunia alfajiri juzi.

MSIMU wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2019/2020 utarejea tena Juni ...

foto
Mwandishi: Na Vicky Kimaro

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi