loader
Picha

RC Pwani asifu mchango wa kampuni

MKUU wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo amesifu juhudi za mmiliki wa Kampuni ya Global Packaging na Wande Printing and Packaging Ltd, Joseph Wasonga za kuchangia shughuli za maendeleo mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hafla fupi ya makabidhiano ya mifuko 200 ya saruji kusaidia ujenzi wa ukumbi na ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani mjini Kibaha, Mkuu wa Mkoa, Ndikilo alisema kuwa Wasonga amekuwa mfano wa kuigwa katika kuchagiza maendeleo katika mkoa wake.

“Kwa kipekee kabisa napenda kumshukuru Mwenyekiti wa Makampuni ya Global na Wande Printing anavyojitoa katika kutimiza malengo ya chama na serikali mkoani hapa jambo linalopaswa kuigwa na kila mwekezaji na wadau wote wa maendeleo,’’ alisema Ndikilo.

Akizungumza mchango wa mifuko 200 ya saruji ambayo ilikabidhiwa kwa ofisi ya CCM Mkoa wa Pwani, Ndikilo alisema ujenzi wa ukumbi na ofisi za mkoa utaongeza fursa Mkoa wa Pwani.

“Mchango huu kwa CCM Mkoa ukitumika vizuri na hatimaye kukamilika kwa ujenzi wa ukumbi na ofisi utachangia kuongeza fursa za ajira, mapato na kuendelea kuimarika kwa CCM ndani ya Mkoa wa Pwani,’’ alisema Ndikilo.

MSIMU wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2019/2020 utarejea tena Juni ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi