loader
Picha

‘Halmashauri zianzishe maktaba karibu na wananchi'

UONGOZI wa Maktaba ya Taifa (TLS) umewataka wananchi kutumia maktaba zilizopo kunufaika kielimu na kupata taarifa mbalimbali. Aidha, umezishauri halmashauri nchini zianzishe maktaba kwenye maeneo yaliyo karibu na wananchi ili wazifikie kirahisi.

Mkuu wa Divisheni ya Ufundi katika maktaba hiyo, Angela Mandala alisema hayo jana jijini Dar es Salaam alipozungumza na gazeti hili. Aliwahimiza wananchi kuwa na mwamko wa usomaji wa vitabu na majarida mbalimbali yanayopatikana katika maktaba hiyo ili kupata maarifa, kuburudika na kujifunza zaidi.

‘’Kwa sasa tuna vituo 43 vilivyotayarishwa kwa kushirikiana na halmashauri kwa lengo la kuwafikia wananchi wengi zaidi,” alisema. Alisema ili kuboresha huduma zake kwa wananchi, maktaba hiyo imegawanyika katika vitengo vya huduma ya watoto wa shule za msingi na sekondari, huduma ya wanafunzi wa kidato cha tano na kuendelea (watu wazima), huduma ya uagizaji, upokeaji na utayarishaji machapisho (ufundi) na huduma ya kutunza vitabu.

Vitengo vingine ni magazeti na machapisho ya zamani. Kuhusu changamoto, alisema hawajaweza kuwafikia wananchi wengi zaidi kwani vituo ni vichache ukilinganisha na ukubwa wa nchi.

“Hii inafanya wengi kushindwa kutumia mak taba kujisomea kwa sababu za umbali. Wakizungumza kwa nyakati tofauti na gazeti hili, watumiaji wa Maktaba ya Taifa ambao pia ni wanafunzi wa sekondari, Laurenciah Lameck kutoka Sengo Academy na Silyvester Chacha wa Azania waliishukuru serikali kwa kuwawekea mazingira hayo tulivu ya kujisomea katika maktaba.

Lameck aliwataka wanafunzi wenzake kutumia maktaba hasa zilizopo katika maeneo yao ili kujifunza mambo mengi zaidi kwani kuna mazingira rafiki kuliko kusomea nyumbani.

Chacha aliiomba serikali na uongozi wa maktaba kununua na kuongeza vitabu vya kiada na ziada vitoshe watumiaji wanapoongezeka. Moja ya mafaniko ya Maktaba ya Taifa yanatajwa kuwa ni uanzishwaji wa Chuo cha Ukutubi kilichopo Bagamoyo, Pwani na tawi la Dar es Salaam.

Uongozi wa maktaba hiyo umetaka wananchi kutumia vyuo vya hapa nchini ili kujipata elimu ya ukutubi katika ngazi za cheti na stashahada.

MSIMU wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2019/2020 utarejea tena Juni ...

foto
Mwandishi: Na Denis Doniminick na Rachel Juliu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi