loader
Picha

Yanga kupindua matokeo kibabe

KAMATI ya Hamasa ya Klabu ya Yanga pamoja na wachezaji wa zamani wa timu hiyo wamepanga kukutana na kikosi cha timu hiyo kukipa morali kuelekea kwenye mchezo dhidi ya Zesco United unaotarajiwa kupigwa September 28 nchini Zambia.

Katika mchezo huo wa marudiano wa Ligi ya mabingwa Afrika Yanga wanahitaji ushindi sare ya kuanzia 2-2 au ushindi wa aina yoyote ili isonge mbele baada ya kulazimiswa sare ya 1-1 na Zesco ya Zambia kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jana, mwenyekiti wa kamati hiyo inayoundwa na wajumbe 18, Suma Mwaitenda alisema lengo la kukutana na wachezaji hao ni kuwatia moyo na kuonesha mashabiki wa timu hiyo wako nyuma yao na wanahitaji matokeo chanya kwenye mchezo huo wakimataifa.

 “Pamoja na hamasa kwa mashabiki wetu, lakini pia tumepanga kukutana na wachezaji wa kikosi chetu kwa kushirikiana na wachezaji wa zamani wa Yanga kuwapa morali nyota wetu kuelekea kwenye mchezo dhidi ya Zesco, ambao kimsingi tunahitaji kupindua matokeo kibabe na kusonga mbele, ” alisema Mwaitenda.

Alisema Licha ya kwamba timu ikipata matokeo chanya inaweza kuchagiza mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani, lakini timu yao hiyo imekuwa haipati matokeo mazuri kutokana na kuwa na kikosi kipya ambacho kinatakiwa kupewa muda.

Alisema pamoja na kukutana na wachezaji wa kikosi hicho ,kamati hiyo imetoa shukrani za dhati kwa wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kwa kujitokeza kwa wingi kwenye michezo iliyopita kuwapa sapoti wachezaji wa kikosi hicho. “

Mpira ni burudani kwenye mchezo uliopita dhidi ya Zesco watazamaji waliojitokeza ni 40,000, lakini bado tunaendelea kuhamasisha wengine 20,000 ili kufika 60,000 kuujaza uwanja, “alisema.

Alisema na wao kama kamati ya hamasa wanafanya maandalizi makubwa kuandaa na kuratibu safari ya kwenda nchini Zambia kwenye kukisapoti kwenye mchezo wa marudiano utakaochezwa katika Uwanja wa Levy Mwanawasa.

BOSTON Marathon sasa imefutwa kabisa ikiwa ni mara ya kwanza ...

foto
Mwandishi: Na Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi