loader
Picha

Mwakyembe aita Watanzania JAMAFEST Uhuru

WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe wamewataka Watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi wa tamasha la utamaduni la Afrika Mashariki (JAMAFEST) litakalofanyika Jumapili kwenye Uwanja wa Uhuru.

Tamasha hilo la siku nane litaanza rasmi Jumamosi na siku inayofuata itakuwa ni ufunguzi rasmi, ambapo linatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya wajasiriamali mbalimbali wa bidhaa za kitamaduni.

Akizungumzia tamasha hilo jana Dk Mwakyembe alisema licha ya kugongana na mechi ya Taifa Stars itakuwa ndio vizuri kwasababu itageuka kuwa kivutio.

“Naita Watanzania waje kwa wingi kujionea bidhaa mbalimbali za kitamaduni bure, kutakuwa na burudani nyingi kutoka kwa wasanii mbalimbali,”alisema.

Alisema miongoni mwa wasanii aliowaalika kwa ajili ya kuburudisha katika tamasha hilo la bure ni Diamond Plutnumz, Hadija Kopa, Rich Mavoko, Lina Sanga na wengine kibao.

Pia, aliwaondoa hofu kuhusu suala la usalama kuwa litakuwepo kwa wajasiriamali na wanaoenda kutembelea mabanda, kwani wamejipanga vizuri.

Waziri alisema kutakuwa na shindano la insha kwa lugha ya Kiswahili zitakazozishandanishwa kwa watoto kuhusu kauli mbiu ya tamasha hilo inayosema ‘Uanuai wa Kitamaduni, Msingi wa Kitengano wa Kikanda, Maendeleo ya Kiuchumi na Kushamiri kwa Utalii’.

BOSTON Marathon sasa imefutwa kabisa ikiwa ni mara ya kwanza ...

foto
Mwandishi: Na Grace Mkojera

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi