loader
Picha

Malinzi atoa utetezi wake kortini

ALIYEKUWA Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa hakuwahi kujaza fomu ya kudai fedha alizokuwa akiikopesha TFF na kwamba alikuwa akilipwa kulingana na utaratibu waliojiwekea kwenye shirikisho hilo.

Alidai hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde wakati akiulizwa maswali na Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai.

Malinzi alidai hajawahi kutoa maelekezo ya upokeaji wa fedha hizo na kueleza kuwa katika mashitaka ya 16 hadi 25 yanaonyesha alilipwa fedha na TFF.

Alidai fedha hizo zililipwa kwa utaratibu na kueleza kuwa hundi na vocha zilizotolewa mahakamani kama ushahidi ni baadhi, kwani zipo nyingine ambazo hazikuletwa mahakamani kama ushahidi.

“Niliwahi kufadhili mbio za wabunge kwa miaka saba, nilipromoti ngumi na nilifadhili mchezo wa golf kwa kutumia fedha zilizotoka Cargo Star, lakini sikuwahi kueleza chanzo cha mapato yake,” alidai Malinzi.

Malinzi bado anaendelea kuhojiwa kutokana na ushahidi wake wa utetezi. Hakimu Kasonde aliahirisha kesi hiyo hadi leo kwa ajili ya kuendelea na hatua ya usikilizaji upande wa utetezi.

BOSTON Marathon sasa imefutwa kabisa ikiwa ni mara ya kwanza ...

foto
Mwandishi: Na Francisca Emmanuel

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi