loader
Picha

IJUMAA: Siku maalum ya kuvaa mavazi ya Afrika Mashariki

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imetangaza siku za Ijumaa kuwa siku maalumu kwa mavazi ya kiutamaduni yanayotengenezwa kwenye nchi wanachama, zikipewa jina ‘Afrika Mashariki Fashion Day’.

Haya yameamuliwa leo, Alhamis kwenye Baraza la 36 masuala ya biashara, viwanda, fedha na uwekezaji (SCTIFI) jijini Arusha.

Baraza hilo limetangaza pia wiki ya kwanza ya mwezi Septemba kila mwaka, kuwa wiki ya mitindo yaani ‘Afrika Mashariki Fashion Week’ huku yakienda sambamba na maonyesho ya Afrika Mashariki ya mavazi yanayotengenezwa kwenye jumuiya hiyo.

Kutokana na suala hili, EAC imetakiwa kuzalisha malighafi husasani ya zao la pamba kwa wingi zaidi ili kukidhi hitaji lilopo la kutengeneza nguo zake.

Akifungua mkutano huo Waziri wa Biashara na Viwanda wa Rwanda Soraya Hakuziyaremye amesema ‘hii ni fursa kwa nchi zetu kuzalisha na kufanya biashara zaidi hasa katika Eneo Huru la Biashara Barani Afrika (AfCTA).”

WANAWAKE wenye matatizo ya Fistula nchini wametakiwa kuacha kujifungia ndani ...

foto
Mwandishi: Na Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi