loader
Picha

Wachina wanavyobandika nembo za China bidhaa kutoka Kibaha

IMEBAINIKA kuwa baadhi ya raia wa China wanaomiliki viwanda wilayani Kibaha wamekuwa wanapotosha kwa kubandika nembo zinazoeleza kuwa bidhaa hizo zimetengenezwa China wakati usahihi ni kuwa zimetengenezwa Kibaha.

Ili kufanikisha mpango wao huo mchafu, wamiliki hao wanadaiwa kuwa wamekuwa wanazisafirisha bidhaa hizo usiku kutoka katika viwanda vyao mbalimbali Kibaha hadi Kariakoo na kuziweka madukani zikionesha kuwa zimetengenezwa nchini China.

Siri hiyo imefichuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani, Asumpta Mshama wakati akizungumzia mikakati mbalimbali ya wilaya hiyo kukuza sekta ya viwanda.

“Tumekuwa na ugomvi na wenye viwanda, usiku wanabandika alama ya bidhaa kuwa zimetengenezwa China na wanasafirisha vitu kutoka hapa kwenda sokoni Kariakoo usiku.

“Unazikuta sahani dukani Kariakoo, unasema sahani hizi ni nzuri na nembo yake inaeleza kuwa imetengenezwa China kumbe imetengenezwa Kibaha, kwani kuna tatizo gani ukisema imetengezwa Kibaha?” alihoji Mshama.

Mshama alisema, wanataka Kibaha iwe Guangzhou kwa kuwa wanazalisha kila kitu. Guangzhou ni mji maarufu kwa biashara nchini China. Mshama alisema ili kufanikisha hilo hadi mwaka 2022 au 2023 haitakuwa rahisi kuitofautisha Kibaha na Dar es Salaam.

Aliyasema hayo wakati akizungumza na timu ya wafanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Maonesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani 2019 na Kongamano la Fursa za Biashara na Uwekezaji mkoani humo.

“Kwa maana hakuna tusichokuwa nacho, kama ni sahani tunatengeneza, kama ni vipodozi tunatengeneza, kama ni magodoro, vituo vyote,” alisema. Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo alisema ujenzi wa viwanda mkoani humo si jambo la siasa, vipo, anayetaka aende kuviona.

Alisema tangu Serikali ya Awamu ya Tano ilipoingia madarakani, mkoa huo ndio unaoongoza kwa ujenzi wa viwanda vipya vikubwa na vya kati. Alisema katika miaka minne ya uongozi wa serikali hiyo, Pwani imejenga viwanda si chini ya 100 vya ukubwa huo.

Alisema, hadi sasa Mkoa wa Pwani una viwanda 1,192 vikiwemo vikubwa, vya kati, vidogo na vidogo. Alitaja miongoni mwa maeneo yenye viwanda kuwa ni Rufiji, Mkuranga, Bagamoyo, Kisarawe, Kibaha na Chalinze.

Alisema, Oktoba Mosi hadi saba mwaka huu kutakuwa na Maonesho ya Pili ya Viwanda Mkoa wa Pwani na pia Oktoba tatu mkoa huo utatekeleza agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa kuwa na Jukwaa la Fursa za Biashara na Uwekezaji.

Mbunge wa Tandahimba, Katani Ahmed (CUF) amejiuzulu kiti ...

foto
Mwandishi: Na Basil Msongo

Weka maoni yako

1 Comments

  • avatar
    Eli Oimer Mollel
    26/09/2019

    Kwani technologiaya kutengeneza hizo bidhaa ni ya Tanzania au ya Wachina.

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi