loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wakamata dawa za kulevya za bil 380/-

NYAMBIZI katika bahari ya Pacific imekutwa ikiwa na zaidi ya dawa za kulevya pauni 12,000 zenye thamani ya dola za Marekani milioni 165 sawa na Sh bilioni 379.5.

Chombo hicho kinachotembea chini ya bahari kilikamatwa na maofisa wa kikosi cha majini wa Marekani, ambapo pia waliwakamata watuhumiwa wanne wa kusafirisha dawa hizo.

Maofisa hao walitumia boti mbili kuifuatilia nyambizi hiyo iliyokuwa na urefu wa futi 400, Septemba 5, mwaka huu.

Katika operesheni hiyo, maofisa hao walibaini pauni 11,000 za cocaine na kiasi kingine cha dawa hizo za kulevya kilishindikana kuchukuliwa kutokana na nyambizi hiyo kutotulia.

“Kazi ya kukamata chombo hiki ilikuwa ngumu kwa kuwa ilifanyika usiku, lakini katika operesheni hii, chombo hiki kilionekana kupitia ndege iliyokuwa ikifanya doria katika eneo hilo,” ilisema taarifa iliyotolewa na kikosi hicho cha majini.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa baada ya ndege hiyo kuiona nyambizi hiyo, majira ya alfajiri kikosi cha doria ya majini kilituma boti zake mbili zikiwa na maofisa na kuifuatilia nyambizi hiyo.

Kamanda wa kikosi cha doria cha eneo hilo, Luteni Kamanda Matthew Kroll alisema vyombo vingi wanavyovikamata hutokea maeneo ya Amerika ya Kusini vikijaribu kuingia Kusini mwa nchi ya Mexico au Amerika ya Kati.

“Kwa hiyo, huko ndio tumewekeza zaidi vifaa vyetu kwa kushirikiana na mataifa mengine ya karibu kwa ajili ya kuzuia biashara hii haramu,” alisema Kroll.

Tukio hilo ni moja ya matukio kadhaa ya kukamatwa kwa dawa za kulevya yaliyofanyika mwezi huu, ambapo kikosi cha doria cha majini cha Seneca nacho kilikamata pauni 12,000 za Cocaine Septemba 20, mwaka huu, jijini Miami.

Aidha, vyombo viwili vya vikosi vya doria vya majini kutoka Tahima na Midgett pia vilikamata pauni 9,000 za dawa za kulevya mapema mwezi huu.

WAANDAMANAJI katika mji wa ...

foto
Mwandishi: NEW YORK, Marekani

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi