loader
Picha

Viwanda Mkuranga neema Dar es Salaam

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga amesema uwekezaji wilayani humo umetoa fursa nyingi za ajira ikiwemo inayowezesha wananchi kupata Sh 7,500/- kila siku kwa kuuza koni jijini Dar es Salaam.

Sanga amesema uwekezaji wilayani humo umewanufaisha Watanzania wengi na kwamba, viwanda Mkuranga vinaajiri wananchi kutoka ndani na nje ya wilaya hiyo wakiwemo wakazi wa Dar es Salaam wanaokopeshwa koni ili wauze wapate faida.

Ameieleza timu kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kuwa, baadhi ya wananchi wametoka kwenye maeneo mbalimbali nchini kwenda kufanya kazi viwandani Mkuranga hivyo uwekezaji ulifanywa hadi sasa umetoa fursa nyingi za ajira.

“Zipo ajira za moja kwa moja na zipo ajira ambazo sio za moja kwa moja. Mathalani ukiangalia kule Dar es Salaam kuna wale vijana wanaotembea na ile mifuko wanauza zile ice cream”amesema. Sanga amesema, kiwanda kilichopo Mkuranga cha kampuni za Bakhresa kimeajiri zaidi ya watu 2,500 wauze koni na kinakusudia kuajiri zaidi ya watu 20,000.

“Na wale vijana ule mfuko wanaotembea nao ule zile bidhaa zina thamani ya shilingi 7,500/- kwa maana kwamba moja ni shilingi 250/- na anakopeshwa, yeye pale anatakiwa akauze apate shilingi elfu kumi na tano maana yake ni mara mbili. Na ile anakopeshwa asubuhi akiuza kwa siku anarudi nyumbani na shilingi 7,500/- ni kazi gani hiyo inayoweza ikakupa fedha hizo. Hayo ni mafanikio ya uwekezaji ndani ya wilaya ya Mkuranga”amesema.

 TANGU mwishoni mwa wiki iliyopita bei ya gesi inayotumika kwa ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo, Mkuranga

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi