loader
Picha

DC aeleza faida za maonesho ya viwanda

Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga, Filberto Sanga amesema maonesho ya kwanza ya viwanda mkoa wa Pwani mwaka uliopita yalikuwa na tija kubwa kwa wawekezaji wilayani humo.

Amesema ofisini kwake kuwa, wilaya hiyo ilikuwa na washiriki wengi na wamejiandaa vizuri kushiriki maonesho ya mwaka huu yanayotarajiwa kufanyika kwa wiki moja kuanzia Oktoba 17.

“Maonyesho ya mwaka jana yalikuwa na manufaa makubwa sana, wawekezaji wetu wengi waliyafurahia na waliyashukuru kwa sababu walipata nafasi kubwa ya kujitangaza na waliweza kufahamika na wengi wigo wa wateja wao umepanuka” amesema Sanga.

Amewaeleza wafanyakazi kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kuwa, Mkuranga itakuwa na washiriki wengi kwenye maonesho ya mwaka huu kwenye uwanja wa CCM Sabasaba.

Ametoa mwito kwa wananchi, wajasiriamali na wawekezaji wakubwa kwa wadogo waende kwenye maonesho hayo kwa kuwa pia watu wengi hawajapata fursa ya kutembelea viwanda wilayani humo.

“Ukifika pale kwenye eneo la maonyesho unaweza ukajua viwanda mbalimbali vinavyotengeneza bidhaa mbalimbali zilizopo ndani ya wilaya ya Mkuranga pia na kuona bidhaa zingine ambazo hazizalishwi ndani ya wilaya yetu ya Mkuranga…pia unaweza ukapata masoko”amesema.

 TANGU mwishoni mwa wiki iliyopita bei ya gesi inayotumika kwa ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo, Mkuranga

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi