loader
Picha

DC ataja mvuto wa Mkuranga kuwekeza

Wilaya ya Mkuranga ina sifa nyingi wanazohitaji wawekezaji na ni sehemu sahihi kuwekeza, Mkuu wa Wilaya hiyo, Filberto Sanga amesema ofisini kwake mjini Mkuranga.

Amesema kiwanda cha aina yoyote kinaweza kujengwa Mkuranga kwa kuwa mahitaji ya msingi yapo na wametenga zaidi ya ekari 10,000 kwenye Kijiji Cha Msufini kata ya Mbezi kwa ajili ya uwekezaji.

“Viwanda vya aina zote zile vinaweza vikajengwa ndani ya wilaya yetu, sifa za wilaya hii kujengwa kwa hivyo viwanda zote zipo. Kwa hiyo hatuna mipaka kwamba hiki usijenge hiki ujenge, tuna mipaka kwamba usijenge kiwanda cha kuzalisha silaha, kiwanda cha kuzalisha gongo na matakataka mengine” amesema Sanga.

Ametaja baadhi ya sifa hizo kuwa ni uwepo wa gesi inayotumika viwandani, maji mengi, ukaribu na bandari ya Dar es Salaam, jirani na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na miundombinu mizuri ya usafiri wa barabara.

“Wilaya yetu imejaliwa kuwa na maji mengi sana. Yapo maji ambayo hayapo kwenye miundombinu ambayo imetengenezwa lakini maji mengi yapo ardhini…huku sisi tupo bondeni kuelekea usawa wa bahari kwa hiyo mito mingi iliyotoka huko milimani inaelekea baharini kwa hiyo popote ukichimba unakutana na maji baridi, maji safi ambayo yamerahisisha uwekezaji wa viwanda” amesema Sanga.

Amewaeleza wafanyakazi kutoka Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) kuwa, wilaya hiyo ina ardhi ya kutosha kwa ajili ya uwekezaji inayopatikana kwa urahisi na kwamba, wananchi wa Mkuranga ni wakarimu na wapo tayari kupokea wawekezaji.

“Maeneo ya uwekezaji bado yapo, watu wanaendelea kuwekeza na bado tuna maeneo mengi ya uwekezaji.”amesema Sanga na kuongeza kuwa Mkuranga kuna nishati ya kutosha kwa ajili ya viwanda.

Amesema ofisini kwake kuwa, Serikali imeongeza kiwango cha umeme unaopelekwa wilayani humo kutoka megawati zisizopungua thelathini hadi megawati 50.

“Hapa ndani ya wilaya yetu ya Mkuranga limepita bomba la gesi linalotoka Mtwara kwenda Dar es Salaam na bahati nzuri wakati wanajenga hilo bomba la gesi walizingatia vitu hivyo vya uwekezaji mathalani waliweka pointi karibu mbili” amesema Sanga na kuongeza kuwa baadhi ya viwanda vinatumia gesi hiyo kwa ajili ya uzalishaji.

 TANGU mwishoni mwa wiki iliyopita bei ya gesi inayotumika kwa ...

foto
Mwandishi: Basil Msongo, Mkuranga

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi