loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wiz Khalifa ajichora uso wa Snoop Dogg

KILA mmoja ana njia yake ya kuonesha heshima na kuhusudu kile anachokipenda, ambapo katika hilo, rapa Wiz Khalifa ameamua kuonesha mapenzi yake ya dhati kwa rafiki yake, Snoop Dogg na kujichora mwilini tattoo ya uso wa mkongwe huyo.

Kama hiyo haitoshi, Khalifa amekwenda mbali zaidi na kujichora tattoo nyingine ya kava ya albamu ya kwanza ya Snoop, Doggystyle iliyotoka mwaka 1993 chini ya Lebo ya Death Row Records.

Rapa huyo alionesha michoro yake hiyo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram na kuandika kuwa hiyo ni kazi mpya kabisa aliyochorwa na rafiki yake Brian Henry akimtambulisha kama moja ya wachoraji mahiri kabisa katika tasnia hiyo.

Khalifa aliyeanza kufahamika kimuziki mwaka 2005 anajulikana kwa urafiki mkubwa aliojenga na Snoop, mara kadhaa akimwita ‘uncle’ kama ishara ya heshima kwa mchango wake katika muziki lakini pia akiongozana nae sehemu mbalimbali na mara kadhaa akieleza kuwa huyo ndiyo mfano wake wa kuuiga katika hatua zake kimuziki.

WAANDAMANAJI katika mji wa ...

foto
Mwandishi: Na Mashirika

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi