loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba waifikiria Azam FC

KIKOSI cha Mabingwa wa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba wanendelea kufanya mazoezi kujiwinda na mchezo ujao wa muendelezo wa ligi hiyo dhidi ya Azam FC unaotarajiwa kuchezwa Oktoba 23 kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Simba ambao hadi sasa wanashika usukani wa Ligi hiyo kwa pointi 12 baada ya kushinda mechi zao zote nne zilizopita, wanaendelea na mazoezi makali kwenye viwanja vya Gymkhana kujipanga na mchezo huo ili kulinda rekodi ya kuendelea kupata pointi tatu.

Akizungumza jana, Meneja wa kikosi hicho, Patrick Rweyemamu (pichani) alisema baada ya kutoka kupata ushindi kwenye mechi mbili za kanda ya Ziwa wameingia kambini haraka kujipanga na mechi hiyo.

“ Ratiba yetu inaonesha mchezo unaofuata tutacheza dhidi ya Azam FC Octoba 23, ambapo ligi itasimama kupisha kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA) kwa mechi za kirafiki pamoja na mechi za Kombe la Chan, “alisema Rweyemamu

Alisema awali ratiba ya ligi hiyo ilionesha watacheza na timu ya Halimashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC), lakini hata hivyo yalifanyika marekebisho na mechi inayofuata watacheza na Azam FC.

Rweyemamu alisema pamoja na wachezaji wao wengi watajumuishwa kwenye kambi ya Stars kujiwinda na mchezo huo wa marudiano, bado wanataendelea na kambi hiyo kujipanga vilivyo kwa ushindi.

Hadi sasa miamba hiyo imefanikiwa kuvuna pointi 12 kutoka kwa timu za JKT Tazania 3-1, Mtibwa Sugar 2-1, Kagera Sugar 3-0 kisha Biashara United mabao 2-0 huku wakiruhusu nyavu zao kutikiswa mara mbili tu.

Naamka asubuhi,  sioni kilongalonga, 
Napapasa kitandani,  hamadi hiki hapa,  

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi