loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waziri ataka vyama imara vya wavuvi

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amezindua Ushirika wa Wavuvi katika Mwalo wa Igombe jijini Mwanza na kumuagiza Katibu Mkuu Uvuvi kuhakikisha ifikapo Desemba 31, mwaka huu kuwepo na vyama imara vya ushirika visivyopungua 20 kwenye maeneo yote nchini ambako shughuli za uvuvi zinafanyika.

Huo ni mkakati wa serikali kuwainua wavuvi kutoka kwenye uvuvi wa kujikimu kwenda kwenye uwekezaji mkubwa utakaowezesha kubadilisha maisha yao na kukuza uchumi wa nchi.

Hatua hiyo inakuja baada wavuvi kudharauliwa kwa muda miaka mingi kutokana na shughuli wanayoifanya ambako taasisi za fedha ziliwadharau kuwa hawakopesheki na wala hawawezi kupewa mikopo huku wachuuzi wa mazao ya uvuvi wakiwa ni matajiri wakubwa, lakini wale wanaoingia majini kuvua wameendelea kuwa maskini.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Chama cha Ushirika wa Wavuvi Igombe Limited Ilemela jijini Mwanza, Mpina alisema serikali ya Rais John Magufuli imekataa wavuvi na shughuli za uvuvi kudhauriwa tena ndio maana inatilia mkazo suala la ushirika na kuwaunganisha na taasisi za kifedha na kuanza kukopeshwa.

Alisisitiza sasa wavuvi wanatoka kwenye kupuuzwa na kudhauliwa wanaingia kwenye kundi la kuheshimiwa na kupewa heshima inayostahili kulingana na shughuli yao ambayo Taifa inaitegemea kukuza uchumi na kuipatia nchi fedha za kigeni ambapo mauzo ya samaki nje ya nchi yamefikia Sh bilioni 691 kutoka Sh bilioni 379 mwaka 2018 na kulifanya zao la samaki kuongoza kwa kuipatia nchi fedha za kigeni.

Pia kutokana na kazi kubwa iliyofanywa na serikali ya kukuza sekta ya uvuvi na kuwaendeleza wavuvi, uagizaji wa samaki kutoka nje ya nchi umeshuka kwa kiwango kikubwa kutoka wastani wa Sh bilioni 56 mwaka 2017 hadi kufikia Sh bilioni 17 mwaka huu.

Alisema ushirika huo wa Igombe una mtaji wa Sh milioni 20 zilizotokana na mchango wa wanachama wenyewe, Sh milioni 7.5, Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) imewachangia Sh milioni 10 na Mbunge wa Ilemela ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula amechangia Sh milioni 2.5.

KAYA zilizobainika kuwa na historia ya kutochukua mara ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Mwanza

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi