loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Walemavu watakiwa kujiunga wakopeshwe

NAIBU Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia watu wenye ulemavu, Stella Ikupa amewataka watu wenye ulemavu kujiunga katika vikundi na kuwa wabunifu ili kupata mikopo kutokana na fedha asilimia mbili zinazotengwa kwa ajili yao.

Ikupa alitoa onyo hilo mwishoni mwa wiki alipokuwa akizindua mafunzo ya wajasiliamali kwa makundi ya watu wenye ulemavu yaliyofanyika katika kata ya Buigiri, Wilaya ya Chamwino, mkoani Dodoma.

  “Naomba muunde vikundi na muwe wabunifu ili muweze kupatiwa mikopo itakayowawezesha kujiari na kuwaajiri wengine,” alisema na kuongeza.

“Ninawaomba mjikite kwenye kilimo cha kisasa ambacho kitawaondolea kwenye changamoto mnazokabiliana nazo badala ya kukaa barabarani na mitaani.”

Ikupa aliwataka watu wenye ulemavu wanaokopeshwa mikopo popote nchini kuhakikisha wanaitumia vizuri kwa malengo ya maendeleo kwa sababu fedha hizo hazitolewi kama ruzuku zinatakiwa kurudishwa. Alisema mikopo hiyo inayotolewa kwa kundi la watu wenye ulemavu, ifahamike kwamba inatolewa kwa lengo la kuwawezesha ili waondokane na umasikini, hivyo itumike kwa malengo yaliyokusudiwa ya kuondoa umasikini wa kipato. Hata hivyo, aliwataka watu wenye ulemavu kuachana na tabia ya kukaa barabarani na mitaani, na kutegemea kuomba omba toka kwa wasamaria wema, badala yake watumie nafasi hiyo kubuni miradi ambayo itakayowafanya kujipatia kipato. Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Taasisi isiyo kiserikali ya ‘Nakua na Taifa Langu’ ambaye ni mratibu wa mafunzo hayo kwa makundi ya watu wenye ulemavu, Jessica Mshama alisema, mafunzo hayo yanafanyika kwa malengo ya kuwawezesha kufanya shughuli mbalimbali zinazoweza kuwapatia kipato bila kujali aina ya ulemavu walionao. Mshama alisema, katika jamii walemavu wengi wamekata tamaa na kuona kuwa mlemavu hawezi kufanya shughuli yoyote na kwa mafunzo hayo ni imani yangu kila mmoja atapatiwa elimu ya ufundi kutokana na aina ya ulemavu alionao. Mkurugenzi huyo ambaye ni mjasiliamali alisema, baada ya mafunzo hayo, kundi hilo la watu wenye ulemavu litafanya kazi kwa vitendo na baadhi yao bidhaa watakazojifunza nakusalishwa wataingia kwenye ushindani ya masoko ya ndani na nje. Naye Yusuph Mnyabahi akizungumza kwa niaba ya watu wenye ulemavu alisema, pamoja na mafunzo watakayopewa,wanaiomba serikali kuwatafutia soko la bidhaa wanazozalisha ili wasikate tama kutengeneza bidhaa nyingine.

KAYA zilizobainika kuwa na historia ya kutochukua mara ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Chamwino

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi