loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waziri atoa somo Msalaba Mwekundu

CHAMA cha Msalaba Mwekundu Tanzania kimeshauriwa kuja na mfumo mpya utakaowezesha kupata wanachama kuanzia shule za msingi hadi vyuoni ili kukuza kizazi ambacho kinatoa msaada wa kibinadamu na kijamii kwa maendeleo endelevu.

Ushauri huo ulitolewa jijini hapa na Waziri wa Katiba na Sheria, Balozi Dk Augustine Mahiga wakati akifungua mkutano mkuu wa uchaguzi na akisisitiza kuwa viongozi wapya kuzingatia misingi 7 ya chama hicho na kamwe wasikitumie kwa maslahi binafsi.

Alisema idadi ya wanachama wa chama hicho takribani 20,000 nchi nzima yenye wananchi zaidi ya milioni 50 ni idadi ndogo na kuwataka kuja na mfumo wa kuweza kuwapata wanachama wapya hasa vijana ili angalau wafike milioni moja.

“Lazima muje na mkakati wa jinsi ya kusajili wanachama katika shule za msingi na kuja juu kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, kwa kufanya hivi, kutawafanya watoto na vijana wakalelewa na kukua katika maadili ya utoaji huduma za kibinadamu,” alisema.

Alisema ni lazima chama hicho kikawalenga vijana ili kuongeza nguvukazi ambayo itatoa msaada na huduma za kibinadamu katika kila kona ya nchi pale inapohitajika hususani kwa wazee ambao pia wanahitaji msaada ya kibinadamu.

Aidha, Dk Mahiga alisema uongozi uliochaguliwa unapaswa kuongoza chama kwa kuzingatia misingi saba ya maadili hususani kuzingatia ubinadamu, uadilifu na usawa na wakati wa kutekeleza majukumu yao ili matokeo yanayotarajiwa yapatikane.

Dk Mahiga alisema viongozi hao wanatakiwa kupimwa kwa jinsi bora ya kutekeleza majukumu yao kwa msingi wa uwazi, utawala bora na uwajibikaji huku akisisitiza suala kudhibiti matumizi yasiyo sahihi ya fedha za michango ya wanachama.

Alisema Chama cha Msalaba Mwenguni ni chama ambacho serikali inakitegemea katika kusaidia kufikisha huduma za kiafya na majanga kwa jamii ya Watanzania.

Awali, Mwenyekiti wa Chama cha Msalaba Mwekundi Tanzania, Mwadini Jecha alisema wataendelea kufanya kazi kwa karibu na serikali kusaidia huduma wakati wa majanga.

Pia alitumia fursa hiyo kulishukuru Bunge na Serikali kwa kuwezesha uwepo wa sheria ambayo inakipa nguvu zaidi chama hicho katika kutimiza majukumu yake ndani ya Tanzania.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi amekiomba chama hicho kuangalia namna ya kuhamishia makao yake makuu jijini Dodoma ikiwa ni katika kuunga mkono juhudi za serikali za kuhamia Dodoma na pia kuwa rahisi nyakati ya kutoa misaada ya kibinadamu wakati wa majanga ukiwa unatokea mkoani hapa.

KAYA zilizobainika kuwa na historia ya kutochukua mara ...

foto
Mwandishi: Anastazia Anyimike

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi