loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tambwe: Yanga watapata raha kwa Molinga

Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Amissi Tambwe amesema David Molinga ‘Falcao’ ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kucheka na nyavu ispokuwa anahitaji kupewa muda ili kuthibitisha hayo.

Kocha Mwinyi Zahera amekuwa akibebeshwa lawama kuhusiana na kuwaachia kuondoka Yanga, Tambwe na Heritier Makambo na kumleta Falcao, mchezaji ambaye ubora wake umekuwa ukitiliwa shaka.

Alhamisi iliyopita, Molinga alitoa mchango mkubwa kwa Yanga katika sare ya mabao 3-3 dhidi ya Polisi Tanzania Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam akifunga mabao mawili.

Tambwe ambaye kwa sasa anakipiga Fanja ya nchini Oman, amesema amemfuatilia mchezaji huyo katika mechi kadhaa ambazo ameichezea Yanga na kubaini ana vitu isipokuwa ukubwa wa mwili ndiyo unamnyima uhuru.

 “Kweli Yanga imeonesha udhaifu kwenye ufungaji, lakini watu hawapaswi kumlaumu kocha amemleta Molinga, wampe muda ni mchezaji mzuri anayeweza kumaliza tatizo lililopo kama atazoea mazingira, nimeona staili yake ya uchezaji ni mtu hatari kwenye ufungaji wawe watulivu tu,” amesema Tambwe.

Mshambuliaji huyo amesema kucheza Yanga au Simba inahitaji utimamu wa mwili na mazoezi ya kutosha ili kuhimili presha ya mashabiki, na kwamba hata yeye iliwahi kumtokea wakati alipojiunga na Simba kwa mara ya kwanza.

 Alisema Molinga anatakiwa kuwa na moyo wa chuma na kufanya juhudi za kupandisha kiwango chake, huku Zahera akipambana kumsaidia ili aweze kurudi kwenye uwezo wake kwa sababu yeye ndiyo mtu anayemfahamu vizuri.

SERIKALI imesema mashabiki 30,000 pekee ndio watakaoruhusiwa kushuhudia mpambano wa ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi