loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tovuti EAC kutafuta masoko Ulaya

JUMUIYA ya Afrika Mashariki (EAC) imezindua tovuti ya pamoja kati yake na Umoja wa Ulaya (EU) yenye lengo la kufungua masoko katika nchi za Ulaya kwa wafanyabiashara na wawekezaji wa nchi za jumuiya hiyo.

Tovuti hiyo ilizinduliwa wiki iliyopita katika mkutano wa mtangamano wa kibiashara uliofanyika mjini Nairobi nchini Kenya. Tovuti hiyo pia itafungua masoko kwa wafanyabiashara na kampuni za Ulaya kwa nchi za Afrika Mashariki.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika Mashariki nchini Kenya, Dk Margret Mwakima na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Afrika Mashariki nchini Burundi, Balozi Jean Rigi, walifanya uzinduzi huo na kuwataka wafanyabiashara wa Afrika Mashariki kuchangamkia fursa hiyo.

Mkurugenzi Mkuu wa Forodha na Biashara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Kenneth Bagamuhunda, alisema kuna umuhimu wa kuunga mkono mnyororo wa thamani hasa katika sekta ya kilimo na kuimarisha ubora na ushindani hasa kwa bidhaa kutoka katika nchi wanachama wa EAC.

Meneja wa Programu wa shirika la Ujerumani la GIZ linalojishughulisha na masuala ya ufundi, Dk Kirsten Focken, alisema tovuti iliyozinduliwa itawezesha wafanyabiashara kutoka Afrika Mashariki kufikia soko la Ulaya kwa kutumia ubunifu wao.

Umoja wa Ulaya umeipongeza Jumuiya ya Afrika Mashariki kutokana na ubunifu wake uliowezesha wafanyabiashara wa nchi wanachama kuingia katika soko la Ulaya na kufanya uwekezaji unaonufaisha mataifa ya Ulaya na eneo hilo.

Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Jocelin Cornet, alisema tovuti hiyo ni fursa kwa wawekezaji na wafanyabiashara wa Afrika Mashariki kulitumia soko la Umoja wa Ulaya kupata faida.

“Tovuti hii ni sehemu ya juhudi za Umoja wa Ulaya za kushirikiana na bara la Afrika, ambapo kutakuwa na ubadilishanaji wa taarifa za kibiashara na masoko kati ya umoja huo na Afrika Mashariki,” alisema Cornet. Nchi wanachama wa EAC zilizoshiriki uzinduzi huo ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi.

RAIS Evariste Ndayishimiye (pichani) amewaapisha mawaziri wapya 15, ambao kwa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi