loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Stars yaanza kuiwinda Sudan

TIMU ya soka ya taifa, Taifa Stars leo inatarajiwa kuanza mazoezi kujifua na mechi ya kirafi ki ya Fifa dhidi ya Rwanda na ile ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani, Chan dhidi ya Sudan.

Stars inatarajiwa kucheza na Rwanda Oktoba 14 katika mechi ya kirafiki ya kalenda ya Fifa na siku nne baadaye itacheza na Sudan. Kocha mMsaidizi wa Stars, Juma Mgunda alisema timu hiyo itafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Stars ina kazi ya kupindua matokeo katika mechi dhidi ya Sudan baada ya kukubali kufungwa bao 1-0 nyumbani.

Mshindi wa mechi hiyo atafuzu fainali za Chan mwakani zitakazofanyika Cameroon. Mgunda alisema wachezaji 29 walitarajia kuanza kuripoti kambini tangu jana.

“Mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Rwanda tunategemea yataanza kesho ( leo) Uwanja wa Uhuru ,wachezaji wote walioitwa watakuwa wamewasili kambini kulingana na ratiba ilivyowataka isipokuwa wale wa kutoka nje ya nchi tunatarajia kuungana nao siku tatu zijazo,”alisema Mgunda.

Mgunda alisema anaamini kambi hiyo itakuwa na mafanikio makubwa ya kupata ushindi katika mchezo huo licha ya kusaliwa na siku chache kabla ya kukutana na Rwanda. Alisema katika mchezo huo wanahitaji zaidi ushindi kurudisha moyo kwa watanzania baada ya kupoteza mchezo uliopita nyumbani.

SERIKALI imesema mashabiki 30,000 pekee ndio watakaoruhusiwa kushuhudia mpambano wa ...

foto
Mwandishi: Tuzo Mapunda

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi