loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

De Gea aponda kiwango Man U

KIPA wa Manchester United, David de Gea (pichani) anasema kiwango kinachooneshwa na timu hiyo msimu huu “hakikubaliki kabisa” na hiki ni kipindi “kigumu zaidi” alichowahi kukishuhudia tangu alipojiunga na klabu hiyo.

Mashetani hao wekundu walipokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Newcastle United Jumapili na kuendeleza mwanzo mbaya wa msimu katika kipindi cha miaka 30. Baada ya kipigo hicho, Man United kimsimamo wako katika nafasi ya 12 katika Ligi Kuu, pointi mbili juu ya ukanda wa kushuka daraja.

“Kiwango chetu cha mchezo hakikubaliki kabisa,” alisema De Gea, ambaye ni mchezaji wa kimataifa wa Hispania mwenye umri wa miaka 28. “Msimu mzima kwetu haukubaliki kabisa.”

Akizungumza na Sky Sports, aliongeza: “Hatukutengeneza nafasi yoyote ya maana. Tuna mambo mengi ya kuimarisha. Kwa kweli sijui nini cha kusema. Tunatakiwa kufanya kazi kweli

. “Tuna majeruhi. Sisi ni Manchester United. Tunatakiwa kufanya mazoezi kwa bidii ili kuweza kupambana na kurejea katika kushinda mechi.”

NINI KIMETOKEA Kiungo Matty Longstaff, 19, alifunga bao pekee katika mchezo wake huo wa kwanza wa Ligi Kuu na kuiwezesha Newcastle United kupata pointi katika mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa St James’ Park. Kipigo hicho kinaifanya Manchester United kuendelea kutoshinda ugenini katika mechi nane za Ligi Kuu, baada ya kushinda kwa mara ya mwisho walipopata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Crystal Palace Februari 27.

Ni kipigo kibovu kabisa tangu mwaka 1989. Kikosi cha Ole Gunnar Solskjaer kitawakaribisha vinara wa ligi hiyo, Liverpool Oktoba 20, baada ya kukamilika mapumziko ya kupisha mechi za kimataifa.Kwa De Gea, ni kipindi kigumu zaidi kwake tangu alipojiunga na klabu hiyo yenye maskani yake Old Trafford akitokea Atletico Madrid mwaka 2011. Mhispania huyo alishinda taji la Ligi Kuu katika msimu wa mwisho wa mwisho cha kocha Sir Alex Ferguson mwaka 2013.

Na tangu wakati huo, walimaliza wa pili mara moja na walishindwa kulipigania taji. Kipa huyo amefanya kazi na makocha wanne wa kudumu na wawili wa muda katika kipindi hicho, akiwemo Solskjaer, aliyeteuliwa Machi baada ya kufanikiwa akiwa kocha wa muda,. Alipoulizwa timu hiyo inahitaji nini ili kuimarika zaidi, De Gea alijibu: “Kila sehemu inahitaji maboresho. Kuna mambo mengi ya kuimarisha.”

SERIKALI imesema mashabiki 30,000 pekee ndio watakaoruhusiwa kushuhudia mpambano wa ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi