loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bosi Benki M kurudisha bil 6/-

MKURUGENZI Mkuu wa Benki M (Tanzania), Sanjeev Kumar (63) ni miongozi mwa washitakiwa saba waliokiri makosa na kutakiwa kulipa fidia ya zaidi ya Sh bilioni sita katika mashitaka yaliyokuwa yakimkabili.

Washitakiwa hao saba wamekiri mashitaka ya uhujumu uchumi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu,Dar es Salaam hivyo na hivyo kuiingizia serikali mabilioni ya fedha baada ya kukiri makosa yanayowakabili kutokana na maelekezo yaliyotolewa na Rais John Magufuli hivi karibuni.

Washitakiwa wote wanaokiri na kutakiwa kulipa fedha huziingiza katika akaunti maalumu iliyofunguliwa katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Mwingine ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Aste Insurance Brokers, Astery Ndege ambaye naye alikiri kuisababishia serikali hasara.

Pia wamo wafanyabiashara David Mudi na wenzake wanne, ambao nao walihukumiwa kulipa fidia ya Sh milioni 40 baada ya kukiri kujihusisha na nyara za serikali bila kibali. Mahakama ilimtaka Kumar kuilipa fidia hiyo ndani ya miezi 24 ambapo mpaka sasa tayari ameshalipa Sh milioni 690.

Hatua hiyo, inakuja baada ya upande wa mashitaka kumfutia mshitakiwa huyo mashitaka ya uhujumu uchumi na kumsomea mashitaka mawili ya kuisababishia serikali hasara ambapo alikiri kutenda kosa hilo.

Akisoma adhabu hiyo, Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alisema kuwa katika mashitaka hayo mawili mshitakiwa atatakiwa kulipa faini ya Sh milioni moja kwa kila kosa.

Alisema mshtakiwa atatakiwa kulipa fidia ya Sh bilioni 6, 039,103,579 ambapo atailipa kwa miezi 24, kwa kila mwezi atalipia kiasi cha Sh milioni 222.8. Hakimu Shaidi alisema hati ya kusafiria ya mshitakiwa huyo itabaki katika Ofisi za Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) na safari zake zote zitafatiliwa na ofisi hiyo.

Kabla ya kutolewa adhabu, Wakili wa Serikali, Jacqueline Nyantori alidai hawana rekodi ya makosa ya nyuma ya mshitakiwa hivyo, aliomba mahakama itoe adhabu kulingana na makubaliano ili iwe fundisho kwake na wengine

Akisoma makubaliano hayo, Wakili Nyantori alidai kuwa wameingia makubaliano na mshitakiwa huyo baada ya kukiri kosa la kuisababishia serikali hasara, hivyo wameamua kuondoa mashitaka ya kughushi, ya kutakatisha fedha, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kuwasilisha nyaraka za uongo.

Baada ya kusoma makubaliano hayo, Hakimu Shaidi alimuapisha mshitakiwa na kumuuliza kama alisaini kwa hiari yake na kudai alifanya hivyo kwa hiari yake.

Akisoma mashitaka mapya, Wakili Nyantori alidai katika mashitaka ya kwanza, Januari 20,2016 mshitakiwa hiyo akiwa Mkurugenzi Mkuu wa Benki M Tanzania kwa vitendo vyake alivyovifanya aliisababishia Serikali kupata hasara ya Sh. 6, 039, 103,579.

Alidai katika mashitaka ya pili, mshitakiwa huyo anadaiwa Januari 20, 2016 akiwa katika jiji la Dar es Salaam kwa njia ya ulaghai ndani ya Benki M Tanzania akijua ni udanganyifu alijipatia Dola za Marekani 287,000. Katika hatua nyingine, Ndege aliyekuwa akishitakiwa pamoja na Maimu amehukumiwa kulipa fidia ya Sh 293,446,400.23 kama hasara aliyosababisha kwa Nida.

Hatua hiyo imekuja baada ya Ndege kukiri makosa ya kusababisha Nida hasara ya zaidi ya Sh bilioni 1.1 kwa kuandika barua ya kuomba msamaha kwa DPP na kuingia makubaliano.

Hakimu Mkazi Mwandamizi, Salum Ally alisema mshitakiwa atatakiwa kulipa faini ya Sh milioni nne kwa mashitaka mawili yaliyomkabili ikiwemo ya kuongoza genge la uhalifu na kusababisha hasara hiyo.

Alisema kuwa amezingatia kitendo cha mshitakiwa kukiri kosa lake na sheria inayoelekeza mshitakiwa kulipa faini. Washitakiwa wengine katika kesi hiyo ni Meneja Biashara wa NIDA, Avelin Momburi na Ofisa Usafirishaji, George Ntalima, Mkurugenzi wa Sheria, Sabina Raymond na Xavery Kayombo

KAYA zilizobainika kuwa na historia ya kutochukua mara ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi