loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mpinzani wa Yanga CAF leo

WAPINZANI wa Yanga kwenye mechi ya mtoano ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika wanatarajiwa kujulikana leo itakapochezeshwa droo mjini Cairo, Misri.

Mbali na droo hiyo, pia itachezeshwa droo ya makundi ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Yanga inashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho baada ya kutupwa nje ya Ligi ya Mabingwa na Zesco United ya Zambia.

Leo, Yanga itafahamu timu itakayokutana nayo katika mchezo wa mtoano kuwania kufuzu hatua ya makundi. Kwa mujibu wa ratiba ya michuano hiyo kutoka kwa Shirikisho la Soka Afrika, CAF, mechi hiyo itachezwa Oktoba 27 mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam kabla ya kurudiana ugenini Novemba 3. Kocha wa Yanga, Mwinyi Zahera alisema yupo tayari kukabiliana na timu yoyote watakayopangwa nayo.

Baadhi ya timu ambazo Yanga inaweza kupangwa dhidi yao ni Paradou AC (Algeria), ESAE (Benin), DC Motema Pembe (DRC) na FC San Pedro (Ivory Coast). Pia zipo Pyramids (Misri), Bandari (Kenya), Bidvest Wits (Afrika Kusini), TS Galaxy (Afrika Kusini), Proline (Uganda) na Triangle United (Zimbabwe).

Yanga inabidi kujipanga ili kufanya vizuri kwenye mechi hiyo na kufuzu makundi kwani tangu msimu huu umeanza inaonekana kuwa na kiwango cha chini hali inayotishia hata ustawi wake kwenye mechi za Ligi Kuu.

SERIKALI imesema mashabiki 30,000 pekee ndio watakaoruhusiwa kushuhudia mpambano wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi