loader
Picha

Mfumuko wa bei wapungua

MFUMUKO wa Bei wa Taifa kwa mwaka ulioishia Septemba, mwaka huu, umepungua hadi asilimia 3.4 kutoka asilimia 3.6 kwa mwaka ulioishia Agosti, mwaka huu.

Kupungua huko kunatokana na bei za bidhaa na huduma kwa mwaka ulioishia Septemba, mwaka huu kupungua ikilinganishwa na kasi iliyokuwapo kwa mwaka ulioishia Agosti mwaka huu.

Hayo yamesemwa jijini hapa jana na Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu na Sensa za Jamii, Ruth Davison, wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya mfumko wa bei kwa ajili ya matumizi ya serikali na wadau wa takwimu.

Alisema kupungua kwa mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia Septemba, mwaka huu, kumechangiwa hasa na kupungua kwa bei za bidhaa zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia Septemba, mwaka jana.

“Baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizopungua bei ni mafuta ya taa kwa asilimia 1.0, petroli kwa asilimia 3.3, majiko ya gesi kwa asilimia 1.5, dawa ya kuulia wadudu nyumbani kwa asilimia 2.2 na mafuta ya nywele kwa asilimia 1.3,” alisema.

Hata hivyo, alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwaka ulioishia Septemba, mwaka huu, umeongezeka hadi asilimia 4.0 kutoka asilimia 3.7 kwa mwaka ulioishia Agosti mwaka huu.

 TANGU mwishoni mwa wiki iliyopita bei ya gesi inayotumika kwa ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Weka maoni yako

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi