loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kondoa warasimisha bodaboda

OFISI ya Mbunge wa Kondoa Mjini, ofisi ya Mkuu wa Wilaya na ofisi ya Mkurugenzi wa Mji wa Kondoa, zimeamua kwa pamoja kurasimisha waendesha pikipiki ndani ya Halmashauri ya Mji Kondoa ili kazi hiyo itambulike na kuthaminiwa kama kazi nyingine.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Kondoa Mjini, Edwin Sannda, kwenye mkutano wa hadhara aliouitisha kusikiliza kero za waendesha pikipiki katika viwanja vya Stendi ya Zamani Kondoa Mjini.

“Tunataka kuwasaidia mtambulike ili mpate mafunzo kwa kushirikiana na wadau wengine ambayo yatawawezesha kupata vyeti na leseni kwani wengi wenu hamna pia kupatiwa elimu ya usalama barabarani kuwaepusha na ajali zinazotokea mara kwa mara,” amesema.

Sannda alisema pia watawasaidia waendesha bodaboda kupata mikataba na wamiliki wa vyombo hivyo ili waweze kupata haki zao bila ya kunyonywa.

Ofisa Usalama Barabarani wilayani humo, Inspekta Haule, aliwataka waendesha pikipiki kuzingatia kanuni na taratibu za usalama barabarani ili kuepuka ajali na kupigwa faini za mara kwa mara.

KAYA zilizobainika kuwa na historia ya kutochukua mara ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

1 Comments

  • avatar
    KARIM H GEORGE
    09/10/2019

    HONGERA SANA KIONGOZI KWA UAMUZI HUO NATEGEMEA HATA VIONGOZI WENGINE WA MAENEO YOTE WATAFUATA NYAYO ZAKO WADAU WA BODABODA NA VIONGOZI WENU INABIDI KUFATA TARATIBU ZOTE ILI NANYI MSIWE KERO KWA JAMII PIA MATUMIZI MABOVU YA BODABODA KAMA WIZI WA NAMNA YEYOTE AU UVUNJAJI WA SHERIA ZA BARABARANI HIVI HUPELEKEA NINYI KUWA TATIZO. FATENI SHERIA.

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi