loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba kunoa makali kwa Bandari

MABINGWA wa soka Bara, Simba wanatarajiwa kucheza mechi ya kirafi ki na Bandari ya Kenya Jumamosi ya wiki hii kwneye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Simba inacheza mechi hiyo ikitumia mapumziko ya kupisha michuano ya kimataifa pamoja na mechi za kirafiki za kalenda ya Fifa. Kwa mujibu wa taarifa ya Simba jana, inatarajiwa kucheza mechi tatu za kirafiki kabla ya kuendelea na ligi Oktoba 23 mwaka huu.

Taarifa hiyo ilisema, baada ya kumenyana na Bandari, vinara hao wa Ligi Kuu watasafiri mpaka Kigoma kucheza na Mashujaa FC Oktoba 14 kabla ya kucheza na mabingwa wa Burundi, Aigle Noir FC siku mbili baadae. Mechi hiyo zote zitachezwa Uwanja wa Lake Tanganyika.

Katika mechi hizo, Simba SC itawakosa mabeki Shomari Kapombe, Gadiel Michael, Mohammed Hussein na Erasto Nyoni. Wengibe watakaokosekana ni viungo Jonas Mkude, Mzamiru Yassin na washambuliaji ni Miraj Athumani ambao wapo kwenye kambi ya Taifa Stars na Meddie Kagere anayekwenda kwenye kambi ya timu yake ya taifa ya Rwanda ‘Amavubi’.

Simba haikufanya vizuri kwenye mechi za kimataifa msimu huu baada ya kuishia hatua za mwanzoni. Kwa sasa ndio inaongoza msimamo wa Ligi Kuu ikiwa na pointi 12 katika mechi nne ilizocheza.

SERIKALI imesema mashabiki 30,000 pekee ndio watakaoruhusiwa kushuhudia mpambano wa ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi