loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kigwangalla apongeza wahifadhi, askari kukomesha ujangili

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dk Hamis Kigwangala amewapongeza askari na wahifadhi nchini kwa jitihada wanazofanya za kupambana na ujangili. Alisema juhudi zao hizo zimesababisha ujangili kupungua kwa asilimia 80 na kusambaratisha mitandao ya ujangili.

Ametoa pongezi hizo wakati akizungumza katika sherehe ya kuhitimisha mafunzo ya awali ya jeshi ussu kwa watumishi 112 kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro.

Dk Kigwangwala amesema wahifadhi na askari wamekuwa na bidii na ubunifu katika kukabiliana na ujangili kwa nguvu zao zote na kufanikiwa kusambaratisha mitandao yao na kupunguza kwa zaidi ya asilimia 80.

“Kimsingi ni kama ujangili umeishakoma hapa nchini kwa sababu kesi tunazopata sasa hivi, zaidi ni meno ya tembo ambayo yalipigwa miaka mingi sana, miaka 10, miaka minane nyuma”alisema Waziri Kigwangwala.

Alisema Asilimia 20 iliyobaki ni tembo ambao wanauawa kwa bahati mbaya kutokana sababu mbali mbali na hakuna meno ya tembo wapya waliouawa. Vile Vile Kigwangwala alisema Uwanda wa Mbulu- Mbulu ulioko mkabala na hifadhi ya Msitu mkuu wa Nyanda za Juu Kaskazini wilayani Karatu, Mkoani Arusha, utaanza kutumika kama kambi maalumu ya mafunzo ya ulinzi ya Jeshi Ussu.

Dk Kigwangwala alisema hadi sasa Serikali imekuwa ikitegemea kambi ya Mlele iliyoko wilayani Mpanda, Mkoani Katavi kwa ajili ya kuendesha mafunzo ya jeshi Ussu. Kituo cha Mbulu- Mbulu kitakuwa cha pili.

WADAU wa kili- mo cha mwani wa Kata ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Karatu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi