loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waandishi redio jamii wajifunza kuripoti majanga

WAANDISHI wa habari kutoka kanda zote nchini ambao wanahudumu katika redio za jamii, wameingia katika mafunzo ya siku 5 mjini hapa kujifunza namna bora ya kuripoti maafa na kusaidia wananchi kutambua umuhimu wa kuokoa na pia kudhibiti maafa na majanga mengine.

Katika mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) chini ya udhamini wa Shirika la Maendeleo la Uswisi (SDC) washiriki wanajifunza namna ya kuripoti maafa na pia mfumo wa kitaifa wa kukabiliana na majanga.

Akizungumza mjini hapa Mratibu wa Mradi wa SDC kutoka UNESCO Christophe Legay, amesema kwamba kutokana na kuongezeka kwa majanga na uelewa duni wa wananchi, UNESCO imeona vyema kufunza wanahabari ili waweze kuelimisha jamii.

Alisema kwamba mafunzo hayo ni ya tatu kwa waandishi wa habari na yamegusa wale ambao hawajawahi kupatiwa mafunzo hayo.

“Tunataka wananchi watambue namna ya kukabiliana nayo majanga hayo, ili kusaidia kufikisha taarifa sahihi kwa jamii ambayo wanaitumikia” alisema Legay na kuongeza kuwa wanapowanoa waandishi wamelenga kuwawezesha kuwa na namna bora ya kuandika habari za majanga ili kusaidia kuokoa na kujipanga lisitokee tena.

Alisema kwa sasa wengi wa waandishi namna yao ya kuandika hairidhishi na hivyo kuchochea zaidi hasara badala ya kukabiliana na dhiki hiyo na kuokoa maisha na mali. Naye Kevin Robert, mtaalamu wa Sayansi asilia kutoka UNESCO alisema ni wajibu wa waandishi wa habari, kwanza kutambua namna ya kukabiliana na majanga, elimu ambayo itawapa undani wa nini kinatokea, wafanye nini na nani asaidie wawe na taarifa sahihi za kusaidia wananchi.

Robert alisema wanahabari hao kutoka Redio 25 na Mratibu kutoka mtandao wa Redio za Jamii zilizotawanyika nchini kote ikiwamo mikoa ya Lindi,Katavi, Kilimanjaro Mara wanafundishwa mifumo ya upashanaji habari katika maafa, mifumo ya habari, kitengo cha maafa na utaratibvu wake na namna nzuri ya kusaidia waliokumbwa na mafaa.

KAYA zilizobainika kuwa na historia ya kutochukua mara ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu , Bagamoyo

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi