loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Walima korosho wapongeza serikali

WAKULIMA wa zao la korosho wameipongeza serikali kwa kuwaletea mfumo wa ununuzi wa bidhaa hiyo kwa njia ya stakabadhi ghalani, bila kutaja bei elekezi ya msimu na kuahidi utaleta tija kwa wakulima hao.

Yamesemwa hayo juzi wakati wa mkutano mkuu wa wadau wa korosho hapa nchini kwa mwaka 2019 uliofanyika mkoani Mtwara ambao ulijadili mafanikio na changamoto mbalimbali za zao hilo.

Hanafi Nahonyo mkulima kutoka kijiji cha Mtopwa wilayani Newala mkoani humo alisema kitendo cha serikali kutotaja bei elekezi katika ununuzi wa zao hilo ni ishara tosha kuwa inamjali mkulima. Isaa Ajabu mkulima wa korosho kutoka kijiji cha Namiyonga wilayani Newala mkoani humo alisema kuwa mfumo huo wa stakabadhi ghalani kwa kiasi kikubwa utasaidia kuboresha uchumi wa wakulima hao.

“Mfumo huu wa ununuzi wa stakabadhi ghalani ndiyo uliotufikisha sisi wakulima hapa tulipofikia kwasababu uko nyuma ulikuwa ununuzi huria kwani mnunuzi alikuwa ananunua korosho kwa bei anayotaka yeye na tumeona kabla na baada ya huu mfumo wa stakabadhi ghalani”, alisema Ajabu.

Hata hivyo kitendo cha serikali kuweka utaratibu wa kuwa na bima ya mazao kwa wakulima utasaidia kumwezesha mkulima kupata pembejeo za kilimo kwa urahisi na bila usumbufu wa aina yoyote.

Naibu Waziri wa Kilimo, Omary Mgumba alisema mfumo unaotumika kuuza korosho kwa kutumia stakabadhi ya mazao ghalani licha ya changamoto zake serikali imeamua kuendelea kuutumia kwa ajili ya kuwakombowa wakulima. Mkutano huo umeshirikisha washiriki mia tano kutoka katika mikoa kumi na saba hapa nchini na matarajio ya serikali katika msimu wa mwaka huu 2019/2020 ni kuzalisha tani 290,000 za korosho.

WADAU wa kili- mo cha mwani wa Kata ...

foto
Mwandishi: Sijawa Omary, Mtwara

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi