loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wakala wa bima wapata tuzo

WAKALA wa bima nchini Milvik Tanzania, inayotoa huduma za bima kupitia simu za mkononi, imepata tuzo ya huduma ya bima yenye ubunifu zaidi kupitia huduma yake ya bima mkononi, inayopatikana kwa watumiaji wa mtandao wa tigo nchini.

Milvik Tanzania ilipewa tuzo na Tanzania Annual Insurance Awards (TAIA) kutokana na ubora wa huduma ya bima mkononi, kwa kuonesha ubunifu kwa watumiaji kwa gharama nafuu na rahisi kutumia.

Meneja wa Milvik, Berengere Lavisse alisema; “tunajivunia kutoa huduma rahisi na bora kwa wateja wa kipato cha chini kwa ushirikiano na mtandao tigo kwa mfumo wa huduma za kifedha.

“Kupitia bima yetu mpya ya kulazwa na watoto, wazazi wanaweza kuwalinda watoto wao kwa matibabu ya kulazwa kwa Sh 750 kwa mwezi kwa kila mtoto, kwa kutumia simu zao, bila kujaza fomu za makaratasi na kwa mfumo rahisi wa malipo kupitia mtandao,”alisema.

“Tunawashukuru wateja wetu ambao wameendelea kutuamini katika kulinda hatima za familia zao na tu- natarajia kuwaletea huduma zenye ubunifu zaidi katika mwaka 2020,” alisema.

“Wanachi wajitokeze kwa wingi, kujiunga ili kuweza kutumia huduma hii, kwani itawasaidia kwasababu ni rafiki kwa watu wa hali ya chini, kuweza kuwasaidia kupata huduma kwa urahisi na kwa garama nafuu na kuepusha vifo vya watoto visivyo vya lazima,”alisema.

Fatma Rajabu, mkazi wa Dar es Salaam alishukuru huduma hii ya bima mko- noni kutoka Milvik, kwani imekuwa msaada kwa mas- kini, ambao hawana kipato kikubwa na kuweza kupata huduma hii kwa urahisi.

“Hapo awali tulikuwa tukipata shida ya watoto wetu, kupata huduma bora, kwa mda sahihi,kutokana, hali duni tuliyonayo na kushinndwa kuhimili gharama za matibabu,ilipelekea watoto wetu kushindwa kupata matibabu na wengine kupoteza maisha,” alisema Fatama.

Milvik na tigo wanashirikiana kuanzia mwaka 2012, katika huduma za bima kupitia mfumo wa makato ya muda wa maongezi, kuanzia mwaka 2015 kupitia mfumo wa huduma za kifedha, kwa njia ya mtandao wa simu za mkononi, mpaka sasa Milvik Tanzania ina wateja hai 120,000, kwa mwaka 2018.

KAYA zilizobainika kuwa na historia ya kutochukua mara ...

foto
Mwandishi: Carlos Mheluka, Tudarco

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi