loader
Picha

TRA yawataka wazalishaji kutumia stempu za kodi za kieletroniki

MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) imewataka wazalishaji wanaotakiwa kutumia stempu za kodi za kieletroniki (ETS) kuendelea kutumia stampu hizo zilizopo kisheria ili waweze kufahamu bidhaa zao halisi zinazoingia sokoni ili kulinda viwanda na walaji wao.

Kamishna Mkuu wa TRA, Dk Edwin Mhede Mhede ameyasema jana alipotembelea Kiwanda cha Uzalishaji wa Bia cha Tanzania (TBL) mkoani Mbeya ili kujione namna stempu za kodi za kieletroniki zinazofanya kazi katika kiwanda hicho.

Alisema ETS inasaidia kukusanya taarifa sahihi si kwa matumizi ya kukadiria kodi pekee bali inamsaidia pia mzalishaji kujua kiasi alichozalisha na kwa muda gani lakini pia itamsaidia kuona kama kuna changamoto yoyote kuifanyia kazi mapema kitu ambacho ni muhimu sana katika shughuli za uzalishaji.

 “Ujumbe wangu kwa wazalishaji wengine ni kwamba waendelee kutumia stampu za kodi za kielektroniki kama ambavyo tumeelekezwa na sheria na taratibu za kodi kwa kuwa inasaidia kuongeza ufanisi katika uzalishaji na kuweka taarifa sahihi za uzalishaji huku zikilinda walaji kwa kupata bidhaa halisi,” alisema.

Kwa upande wake Meneja wa TBL mkoa Mbeya, Godwin Fabian alisema kiwanda chake kinaamini kwamba ETS ni msaada mkubwa kwa wazalishaji kwa kuwa inawezesha kugundua bidhaa zisizo halali na zinazoingia sokoni bila kufuata taratibu za uzalishaji na lakini pia inasaidia katoka ulipaji sahihi wa kodi.

“Ujumbe wangu kwa wazalishaji wengine waone ni kitu kizuri na wasiogope kutumia stempu za kodi kieletroniki kwa kuwa kama bidhaa zote zitawekwa stempu hizi itasaidia kufahamu bidhaa zisizo halali zinazoingia sokoni na hivyo mfumo huu utasaidia kukabiliana nazo,” alisema Meneja huyo.

Kwa mujibu wa TRA, Matumizi ya Stempu za Kielektroniki za Kodi kwa bidhaa zinazotozwa Ushuru wa Bidhaa yalianzishwa kuchukua nafasi ya matumizi stempu za karatasi ambazo matumizi yake yalihusishwa na vitendo vya ukwepaji kodi pamoja na bidhaa bandia kwa kiasi kikubwa.

ILI kukabiliana na ugonjwa wa Covid- 19 unaosababishwa na virusi ...

foto
Mwandishi: Mwandishi wetu, Mbeya

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi