loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Bale achoshwa na vituko Real Madrid

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Gareth Bale, ana hasira na amechoka na vigogo hao wa soka wa Hispania na sasa anataka kuondoka katika klabu hiyo, imeelezwa.

Bale alikuwa amejiandaa kujiunga na klabu ya Ligi Kuu ya China ya Jiangsu Suning kwa mktaba wa miaka mitatu katika kipindi cha majira ya joto, ambapo angekuwa akiondoka na kitita cha pauni milioni 1 kwa wiki.

Hata hivyo, Real Madrid iligoma kukamilisha mpango huo kwa sababu walikuwa wakitaka ada ya uhamisho. Kocha wa Real, Zinedine Zidane, alisema: “Tunatarajia ataondoka haraka iwezekanavyo,” maelezo ambayo yalijibiwa na wakala wa mchezaji huyo, Jonathan Barnett: “Zidane amekosea, hajaonesha heshima kwa mchezaji, ambaye ameifanyia makubwa Real Madrid.”

Bale akiwa na timu hiyo ameshinda mataji manne ya Ligi ya Mabingwa wa Ulaya, moja la La Liga, Copa del Rey na mara tatu la Uefa Super Cup na Kombe la Dunia, huku akiifungia klabu hiyo mabao 100. Baada ya mpango wake wa kwenda China kufeli, mchezaji huyo wa kimataifa wa Wales, mwenye umri wa miaka 30, alijiondoa katika mechi za maandalizi kabla ya kuanza kwa msimu mjini Munich, Ujerumani, ikielezwa kuwa hakuwa vizuri kisaikolojia.

Msimu huu alirejea katika timu hiyo, huku akifunga mara mbili katika mechi saba wakati timu yake ikirejea kileleni mwa msimamo wa La Liga. Lakini mchezaji huyo aliachwa katika mchezo wa wiki iliyopita wa Ligi ya Mabingwa Ulaya walipocheza dhidi ya Club Bruges, kabla ya kurejea katika kikosi cha kwanza wakati waliposhinda 4-2 dhidi ya Granada Jumamosi.

“Gareth Bale amechoka. Hawezi kuendelea kufanya hivi kwa muda mrefu. Ana hasira, amechanganyikiwa,” “ alisema Balague. Wakati Zidane akirejea katika klabu hiyo, aliamua kutoendelea na Bale, bila ya kutoa sababu za wazi.

“Bale amecheza vizuri wiki za hivi karibuni, sababu ana hasira. Kumuacha nje wakati wa mchezo dhidi ya Bruges ni ngumu sana kuelewa na hiyo imemfanya kushindwa kuendelea kuvumilia.”

“Kwa mara ya kwanza tangu atue Real Madrid katika kipindi cha majira ya joto mwaka 2013, mchezaji huyo wa Wales anataka kuondoka. Anahisi hatendewi haki kabisa kwa kile wanachomfanyia,” alisema.

MOHAMED Salah, alifunga mara mbili na kusaidia mabingwa Liverpool kufi ...

foto
Mwandishi: MADRID, Hispania

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi