loader
Picha

Mama, mwanawe wamekufa wakitoka shambani

KAZI ya kuopoa gari baharini lililokuwa limembeba mama na binti yake imechelewa kuanza leo asubuhi kutokana na kasi ya mkondo wa maji na pia kupisha meli zilizotarajiwa kupita kwenye eneo hilo.

Gari hilo Toyota Isis lenye namba za usajili KCB 289C lilizama kwenye Bahari ya Hindi katika eneo la Likoni Septemba 29 saa 12 jioni baada ya kurudi nyuma wakati likiwa kwenye kivuko Mv Harambee.

Wakati wa ajali hiyo gari hilo lilikuwa limembeba Mariam Kighendi (35) na binti yake Amanda Mutheu (4).

Msemaji wa Serikali ya Kenya Cyrus Oguna amesema kazi ya kuopoa gari hilo ilipangwa kuanza leo saa tatu asubuhi lakini kasi ya mkondo wa maji ilihatarisha usalama wa wazamiaji.

Jana jioni Oguna alithibitisha kuwa gari hilo lilionekana umbali wa mita 58 kutoka usawa wa bahari.

Mume wa Mariam, John Wambua amesema, mkewe na mwanawe walizama wakati wanavuka wakitoka shambani kwao Kwale.

Amesema, nusu saa kabla ya ajali hiyo alizungumza na mkewe akamjulisha kuwa yeye na mtoto wao Amanda walikuwa wanajiandaa kuvuka kurudi nyumbani kwao Mombasa.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi