loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Korti yaelezwa mhadhiri alivyonaswa akijiandaa kwa ngono na mwanafunzi

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeelezwa namna Mhadhiri Msaidizi wa Chuo Cha Taifa cha Usafi rishaji (NIT), Samson Mahimbo (68) alivyokutwa akijiandaa kufanya ngono na mwanafunzi wake.

Wakili wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Faraja Sambala aliyaeleza hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wakati akisoma maelezo ya awali ya mshitakiwa.

Sambala alidai kuwa Mahimbo ni mkazi wa Makongo juu Dar es Salaam na wakati wa tukio alikuwa mwajiriwa wa NIT. Alidai mshitakiwa huyo alikuwa akifundisha somo la Usimamizi wa Barabara na Usafirishaji na kwamba mwanafunzi huyo (jina linahifadhiwa) alikuwa miongoni mwa wanafunzi wake.

Ilidaiwa mahakamani hapo kati ya Januari 5 na 11,2017 alitumia madaraka yake vibaya kwa kuomba rushwa ya ngono kutoka kwa mlalamikaji. Sambala alidai Januari 11, alimpigia simu mwanafunzi huyo akimsisitiza wakutane na siku iliyofuata walikutana baa iitwayi Shani iliyopo maeneo ya Mwenge.

“Mshitakiwa alikuwa na mtihani wa marudio ambao (mlalamikaji) alitakiwa kufanya, karatasi ya majibu na marking scheme,” alidai Sambala.

Aliendelea kudai mshitakiwa alimsahihishia na kumpa alama 67 na baada ya kumaliza wakahamia kwenye baa na nyumba ya kulala wageni inayoitwa Camp David , iliyopo Mlalakuwa Mwenge.

Alidai walikunywa na kulewa na kuchukua chumba na kuingia ndani na kwamba mshitakiwa alianza kuvua nguo na kubaki na nguo ya ndani.

“Mshitakiwa alianza kumkumbatia (mlalamikaji) na kuanza kumvua nguo zake na mara walisikia mlango ukigongwa na Mlalamikaji aliufungua na kuingiza maofisa wa Takukuru, mhudumu wa baa na mjumbe. Walikuta nguo zipo juu ya meza,” alidai.

Pia alidai Januari 12, 2017 mshitakiwa alienda kuandika maelezo Takukuru na Agosti 14, mwaka huu aliletwa mahakamani. Mshitakiwa alikana maelezo hayo na kukubali majina yake na mahali anapokaa. Upande wa mashitaka ulidai kuwa wanamashahidi sita na vielelezo saba ili kuthibitisha mashitaka hayo.

Mshitakiwa huyo alidai atakuwa na mashahidi wanne. Mshitakiwa yupo nje kwa dhamana na keshi itaanza kusikilizwa Novemba 11, mwaka huu.

MASHIRIKA mbalimbali ya kimataifa ya usafiri ...

foto
Mwandishi: Francisca Emmanuel

Post your comments

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi