loader
Picha

UWT yahamasisha wanawake kujiandikisha

JUMUIYA ya Umoja wa Chama cha Mapinduzi (UWT) mkoa wa Dar es Salaam umewahamasisha wanawake katika mkoa huo kujitokeza na kujiandisha ili kushiriki kikamilifu katika uchaguzi wa serikali za mitaa.

Mwenyekiti wa UWT, Gaudentia Kabaka alisema hayo jana jijini Dar es Salaam wakati wanawake wa umoja huo walipokutana kwa ajili ya kumuenzi Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.

Kuhusu uchaguzi alisema wanawake wengi wamekuwa wakibaki nyuma kw akutokujua maana ya kujiandikisha bila kujua kuwa ni sehemu mojawapo ya kupata viongozi waona ambao ndio wenye kuwatambulisha kwa ngazi za juu.

“UWT iwe bega kwa bega na wanawake wote wa mkoa huu kuhakikisha wanajitokeza na kujiandikisha ili waweze kupiga kura kuchagua viongozi wao wa mitaa,” alisema Kabaka na kuwataka pia kuwapa motisha wanawake watakaogombea nafasi mbalimbali.

Aliwaambia wanawake hao kutambua kuwa muda wa siku tano uliopangwa wa kujiandikisha ni mdogo sana hivyo ni muhimu kuutumia kikamilifu.

Hata hivyo alikemea upotoshaji unaotolewa na watu katika baadhi ya maeneo nchini kuhusu azma ya kujiandikisha katika uchaguzi huo, kwamba wenye vitambulisho vya kupigia kura hawatakiwi.

“Nimepata ujumbe mfupi kutoka mkoani Tarime kuwa wapo watu wanapita katika nyumba za watu hususani wanachama wa CCm wakiwaambia kuwa wale wenye vitambulisho wasiende kujiandikisha,” alisema.

Kuhusu kumuenzi Nyerere UWT mkoa huo walitoa misaada mbalimbali ya vyakula pamoja na vifaa kwa kituo cha kulelea watoto yatima na wazee cha Mama Teresa kilichopo eneo la Mburahati jijini Dar es Salaam.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa UWT Queen Mlozi aliwataka wanawake wa UWT mkoa huo kutambua kuwa iwapo hawatojiandikisha jitihada za kufikia ushindi zitakuwa ni bure.

Aliwataka wanawake haok uhakikisha wanapita nyumba kwa nyumba, shuka kwa shuka ili elimu ya kujiandikisha iweze kuwafikia wote.

WAKURUGENZI wawili wa Kampuni ya Tanzanite One Mining Ltd ya ...

foto
Mwandishi: Lucy Lyatuu

Weka maoni yako

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi